Rais wa Tanzania, amesema
Serikali inadhamiria kukwamua mchakato wa marekebisho ya katiba, uliokwama kwa
zaidi ya miaka 8, toka mwaka 2014.
Mbali
na hilo Rais Samia ameondoa zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa,
lililodumu kwa zaidi ya miaka 7, tangu mwaka 2015.
Akizungumza
na viongozi wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu Tanzania, Rais Samia
amesema ‘Serikali inadhamiria kukwamua mchakato wa marekebisho ya katiba, kwa
jinsi tutakavyokuja kuelewana huko mbele’, wengine wanasema tuanze na katiba ya
warioba, wengine tuanze na katiba pendekezwa, lakini kuna mambo ya ulimwengu
yamebadilika’,.
Alisema
itaundwa kamati maalumu kwa ajili kutoa ushauri wa namna ya kwenda kupata
katiba ‘si muda mrefu, tutakwenda kuanza na kamati itakayokuja kutushauri,
nataka kusema katiba hii ni ya watanzania si ya vyama vya siasa’,.
Ukiacha
Katiba mpya, kwa muda mrefu nchini kulikuwa na kilio hasa kutoka kwa wanasiasa
na jamii za kimataifa kuhusu haki ya kufanya siasa hasa mikutano ya siasa
kuruhusiwa, ambayo ipo kisheria.
'Hii
ni haki kwa sheria zetu, ni haki kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya
hadhara’, uwepo wangu leo mbele yenu ni kuja kutangaza, lile tangazo la kuzuia
mikutano ya hadhara sasa linaondoka', amesema.
Mikutano
hiyo ilizuiwa muda mfupi baada ya aliyekuwa rais wa awamu ya tano, Hayati John
Magufuli kuingia madarakani kupitia uchaguzi mkuu wa 2015.
'Lakini
ndugu zangu tuna wajibu, wajibu wetu serikali ni kulinda mikutano ya vyama vya
siasa, wajibu wenu vyama vya siasa ni kufuata sheria na kanuni zinavyosema’,
twendeni tukafanye siasa za kistaarabu, tukafanye siasa za kupevuka,
tukafanyeni siasa za kujenga sio za kubomoa, si kurudi nyuma hapa tulipofika,
‘sisi ndani ya CCM tunaamini katika kukosolewa na kujikosoa’, amesema.
Hata
hivyo baada ya Rais Samia kuingia madarakani mwaka 2021, kufuatia kifo cha
Magufuli, alionyesha dhamira ya kuleta maridhiano kwa kuunda kikosi kazi cha
kukusanya maoni.
'Wakati
mnanikabidhi kuongoza nchi hii, busara zilinituma, kwamba jinsi nilivyolipokea
taifa hili, kuna haja ya kufanya taifa liwe kitu kitu kimoja, wote tuzungumze
lugha moja, alisema Rais Samia na kuongeza ' Ili taifa lilwe moja, lazima tuwe
na maridhiano, nikasema kwanza tuwe na mazungumzo kwenye vyama vya siasa'.
Kikosi
kazi kilichoundwa kilileta maoni kwenye maeneo 9, ambapo makubwa matatu
yaliyojitokeza ni kutaka kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa,
mchakato wa katiba mpya na marekebisho sheria mbalimbali.
Rais
amesema tayari michakato ya marekebisho ya sheria imeanza na waziri husika
atakuja kuleta taarifa ya muelekeo.
Wanasiasa,
akiwemo kiongozi Zitto Kabwe wa ACT-Wazalendo akizungumza kuhusu uamuzi wa huo
wa Rais kukwamua mchakato wa katiba na kuruhusu mikutano ya hadhara ya vyama
vya siasa alisema ‘ni hatua kubwa sie tuna furaha, amesimama kwenye maneno
yake’.
Mbali
na Makamu wa rais Phillip Mpango na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, mkutano huo
wa rais na vyama vya siasa uliofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam,
umehudhuriwa na Wenyeviti, makamu wenyeviti na makatibu wakuu na manaibu katibu
wakuu kutoka vyama vote 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu Tanzania.
Vyama
hivyo ni UPDP, NRA, TADEA, TPL, CHADEMA, CUF, NCCR, UDP na UMD.
Vingine ni chama tawala CCM, DEMOKRASIA MAKINI, DP, SAU, AFP, CCK, ADC, CHAUMMA na ACT- Wazelendo.
0 Comments