Header Ads Widget

MATUKIO KATIKA PICHA RPC IRINGA ALLAN BUKUMBI AONGOZA SIKU YA POLISI


kamanda WA polisi WA mkoa wa Iringa Allan Bukumbi akikagua mazoezi ya utimamu wa askari Polisi Leo wakati wa kilele Cha Polisi Day viwanja vya FFU 

Askari Polisi wakionesha utimamu wao 








































Askari 12 watunukiwa Vyeti vya Pongezi kwa kufanya vizuri zaidi Mwaka 2022.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP. Allan L. Bukumbi amewatunuku vyeti vya pongezi Askari Polisi 12 na mtumishi raia mmoja kwa utendaji kazi bora katika majukumu ya kila siku kwa mwaka 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 27 Januari 2023 katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya FFU Kihesa Mjini Iringa, ACP. Bukumbi amesema kazi kubwa ya Askari Polisi ni kuzuia vitendo vya kihalifu katika kulinda raia na mali zao, kwa mwaka 2022 Iringa haikuwa na vitendo vya kutisha vya kihalifu kutokana na Askari na Maofisa walifanya kazi kubwa na ya ziada ya kuzima mitazamo ya kihalifu katika kuzuia vitendo hivyo.

Kamanda Bukumbi amesema askari wote wamefanya vizuri ila waliopewa zawadi ni wawakilishi kutoka kila eneo la utendaji kazi ambao wamefanya kazi vizuri zaidi kwa kujituma na kushirikiana na askari wenzao na wananchi katika kuhakikisha Iringa imekuwa salama kwa mwaka 2022.
 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI