Teddy Kilanga
Arusha
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Taifa, Fadhili Maganya amesema safari za nje ya nchi za Dk Rais Samia Suluhu Hassan zimekuwa na tija nchini hasa katika kuboresha miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu.
Akizungumza wakati akitoa tamko la umoja wa wazazi leo Januari 4,2023 na waandishi habari katika ofisi za CCM mkoa wa Arusha,Mwenyekiti Maganya amesema miradi mingi imetekelezwa kupitia mikopo hiyo licha ya uwepo wa kodi zinazotolewa nchini.
"Ndugu waandishi wa habari sisi sote tunakifahamu vizuri kishwahili hili suala linalozungimziwa nchi nzima la kuhusu safari na mikopo kwa Dk.Rais Samia naomba nitumie maneno haya kwamba Rais anapokwenda nje ya nchi huwa arudi bure,"amesema Mwenyekiti Maganya.
Maganya amesema kuwa kupitia mkopo hiyo sasa hivi changamoto ya madarasa imetatuliwa ikiwa watoto wote wanaostahili wanaenda shuleni wote na wananchi wameondokana na michango mbalimbali waliokuwa kitozwa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa shuleni.
Amefafanua kuwa miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa nchini kuna ambayo inatelelezwa kwa kodi za watanzania lakini pia ipo inayotekelezwa kwa mikopo ambayo nchi inapata kutoka nje kwa juhudi za Mh Rais anaposafiri kwenda huko.
Aidha kuhusiana na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa alitoa wito kwa vyama vya siasa kutumia mikutano hiyo kujenga nchi lakini pia watanzania kumtia moyo na kuunga mkono kwa uamuzi huo kwani umoja na mshikamano ndio msingi wa maendeleo katika nchi.
“Umoja wa wazazi unaviomba vyama vya siasa kuzingatia sheria na kanuni na miongozo mbalimbali katika utekelezaji wa shughuli za siasa hapa nchini na kwa pamoja tuumunge mkono Rais kwa kuendeleza siasa za maridhiano kwa maslahi mapana na mustakabali wa nchi yetu,” amesema Maganya.
Sambamba na hayo jumuiya hiyo imempongeza na kumuunga mkono Rais kwa kuonyesha uongozi madhubuti na imara ambao unaendelea kufanya nchi kuwa na amani na utulivu ambayo ni kuanzisha siasa za maridhiano, mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kuanza kukwamua mchakato wa katiba pamoja na kuendelea kuangalia sheria mbalimbali kwaajili ya kuziboresha.
0 Comments