Header Ads Widget

WAZIRI NAPE AZINDUA 'DATA KILELENI'... AISHUKURU TTCL KWA JITIHADA KUBWA WALIZOZIFANYA..

Na Gift Mongi,MATUKIO DAIMA APP, MOSHI.

Serikali ya Tanzania kwa sasa imeweka rekodi mpya katika nyanja ya kimawasiliano hususani ya intaneti ambayo yana mawimbi yenye  kasi ya mps100 ambayo yamefikishwa katika kilele cha mlima Kilimanjaro ikiwa ni urefu wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari.


Kufikishwa kwa mawasiliano hayo kumeelezwa kuwa kutaenda kuwa na fursa nyingi kwa taifa ikiwa ni pamoja na kutangaza vivutio vya utalii tulivyo navyo na pia kuwawezesha watalii kufanya mawasiliano wakiwa kwenye hifadhi tofauti na kipindi cha nyuma.


Akizindua huduma ya intaneti ijulikanayo kama 'data kileleni' waziri wa habari mawasiliano na teknolojia ya habari, Nape Nnauye amesema Tanzania kwa sasa imeenda kuweka historia ambayo ni jambo la kujivunia katika nyanja za kimawasiliano.


Waziri Nape amesema faida kubwa zitokanazo na mawasiliano hayo ni kuwezesha shughuli za kitalii kufanywa kwa wepesi zaidi kutokana na urahisi wa kimawasiliano lakini pia kuwezesha watalii kufanya shughuli zao wakiwa hifadhini.


"Huduma hii inaenda kuleta mwanga katika sekta ya mawasiliano yaani mtalii atakuwa anatusaidia kutangaza vivutio vyetu lakini TANAPA nao wakifanya shughuli zao kwa urahisi zaidi ambapo wataweza kutumia simu za mezani"amesema 


Amesema uwekaji wa mawasiliano ya intaneti katika kilele cha mlima Kilimanjaro kutasaidia kurahisisha shughuli za kiuhifadhi katika mlima huo pamoja na kurahisisha mawasiliano kwa watalii wanaopanda mlima huo pamoja na wadau wengine.


Kwa mujibu wa waziri Nape ni kuwa Tanzania inakuwa nchi ya kwanza katika bara la Afrika kusimika huduma ya intaneti katika kilele cha mlima Kilimanjaro jambo ambalo ni la kujivunia lakini pia linaendana na kasi ya rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya utalii kama alivyoiasisi kupitia filamu ya'TANZANIA THE ROYAL TOUR'.


"Nitumie nafasi hii pia kulishukuru shirika la mawasiliano la TTCL kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kujenga miundombinu ya mawasiliano ya intaneti  kuanzia Marangu hadi Mandara Kilomita  9.5, Marangu hadi Horombo Kilomita  13, Horombo hadi  Kibo Kilomita 14, Kibo hadi Uhuru Kilomita 5.2, Kibo hadi Uhuru Kilomita 5.2, Kibo hadi Barafu kilomita 3 na kufanya jumla ya kilomita  kuwa 44.7"amesema

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa shirika la TTCL Peter Ulanga amesema mafanikio hayo ni ya kizalendo na imedhihirisha ni namna gani ubunifu unavyoweza kutumika na kuleta manufaa chanya kwenye sekta hiyo muhimu.


"Hapa tumeujulisha ulimwengu kuwa ni namna gani Tanzania imepiga hatua katika nyanja ya kimawasiliano kwa kuweza kufikisha huduma ya data katika mlima Kilimanjaro kwa kutumia mkongo wa taifa"amesema


Msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa akizungumza kwa niaba ya katibu alisema malengo ya wizara hiyo  ni kuhakikisha ifikapo 2025 wananchi kwa asilimia 80 watakuwa wameunganishiwa mfumo wa digitali ikienda sambamba na kukuza matumizi ya tehama.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI