Header Ads Widget

MUAROBAINI WA MBOLEA TANZANIA KUPATIKANA DISEMBA 16 MWAKA HUU

Mkurugenzi wa biashara na maendeleo ya masoko Dokta Kenneth Masuki kutoka kampuni ya Intracom iliyojenga kiwanda Cha mbolea Dodoma
Meneja Biashara na masoko Dokta JULIUS NAMBUA toka kampuni ya Bens Agrostar inayosambaza mbolea za Intracom

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Itracom kutoka Nchini Burundi inatarajia kuzindua kiwanda chenye uwezo wa kuzalisha mbolea tani milioni moja hapo Disemba 16 mwaka huu, hali itakayorahisisha upatikanaji wa mbolea nchini na kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali.


Kiwanda hicho kilichojengwa Dodoma kimetajwa kuzalisha mbolea za FOMI za aina tatu ikiwemo ya kupandia ,kukuzia na kunenepesha pamoja na chokaa ambayo itaenda kuwa tiba kwenye udongo ambao umeharibiwa na tindi kali.


Akizungumza wakati wa kutoa elimu kwa mawakala wa pembejeo za kilimo kutoka mikoa ya Njombe na Mbeya ambayo imefanyika  mjini Makambako Mkurugenzi wa biashara na maendeleo ya masoko wa kiwanda cha mbolea cha itracom Dokta Kenneth Masuki amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha tani milioni moja kwa mwaka.


Meneja wa utafiti na ubunifu wa kiwanda hicho Elias Nyongabo amesema mbolea hizo zina ubora unaotakiwa kwa kuwa zimefanyiwa utafiti kwenye mazao ya Mahindi ,maharage,mpunga, alizeti ,mtama,mihogo na viazi na zimekua na tija kubwa.


Naye Meneja biashara na Masoko kutoka kampuni ya Bens Agrostar Co.Ltd ambayo imepewa kazi ya kusambaza mbolea za Itracom Dokta JULIUS NAMBUA amesema atahakikisha mbolea hizo zinawafikia wakulima kwa wakati ili waongeze kasi ya uzalishaji kwenye mazao yao.


Nao baadhi ya mawakala wa pembejeo za kilimo mkoani Njombe akiwemo Roza Makweta na Ambele Mwaipaja wamesema kiwanda hicho kimekuja wakati mwafaka na kitaenda kuondoa utegemezi wa kutegemea mbolea kutoka nje ya nchi.


Kujengwa kwa kiwanda hicho mkoani Dodoma kunakwenda kuwa muarobaini wa upatikanaji wa Mbolea hapa nchini na kuwakomboa wakulima ambao wamekuwa kwenye changamoto kubwa tangu kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa Corona mwaka 2019 hadi vilipotokea vita vya Ukraine na Urusi.










Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI