Rais wa Cameroon Paul Biya mwenye umri wa miaka 92, ambaye ndiye mkuu wa nchi mwenye umri mkubwa zaidi duniani, amebadilisha safu ya juu ya jeshi katika kile wachambuzi wanasema ni juhudi za kuhakikisha vikosi vya jeshi vinaunga mkono azma yake ya kushinda muhula wa nanebaada ya malalamiko ya umma.
Biya amewateua wakuu wapya wa jeshi la askari wa ardhini, jeshi la anga na wanamaji pamoja na kuwapandisha vyeo mabrigedia wanane hadi nyadhifa za meja jenerali.
Mmoja wa majenerali waliopandishwa vyeo ni mratibu wa kikosi cha wasomi cha Rapid Intervention Battalion (BIR), kitengo maalum ambacho mara nyingi hutumwa katika operesheni za kukabiliana na ugaidi na kuonekana kama msingi wa vyombo vya usalama vya Biya.
Rais Biya pia amemteua mshauri mpya maalum wa rais wa masuala ya kijeshi.
0 Comments