Header Ads Widget

WATU 291 WAACHA KUTUMIA DAWA ZA ARVs MJI WA NJOMBE









************


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wakati Dunia ikiadhimisha siku ya ukimwi kila Disemba mosi ya mwaka,Jumla ya watu 291 kati ya 16,594 wanaotumia dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi ARVS wameripotiwa kutelekeza dawa katika Halmashauri ya mji wa Njombe na kusababisha kuwapo kwa mkwamo wa jitihada za serikali za kupambana na janga la virusi vya ukimwi.

Katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi yaliyofanyika kibena chai kwa halmashauri ya mji wa Njombe imeelezwa kuwa watu hao wameacha kutumia dawa hizo Katika kipindi cha miezi sita hatua ambayo inafifisha jitihada za kuufikia mpango wa 95 tatu ifikapo 2030.

Mratibu wa ukimwi wa halmashauri ya mji wa Njombe Daniel Mwasongwe amesema licha ya serikali na mashirika mbalimbali kuongeza kasi ya kutoa elimu kwa umma juu ya maradhi ya ukimwi lakini bado kuna vikwazo vinajitokeza kwani kuna WAVIU ambao wanaacha kutumia dawa kwasababu mbalimbali ikiwemo ya kiimani baada ya kuombewa na kuaminishwa na viongozi wa dini kuwa wamepona.

Mbali na changamoto hizo idara ya afya halmashauri ya mji wa Njombe imekiri kupata mafanikio kwa baadhi ya maeneo katika mapambano dhidi ya maambukizi mampya ambapo imesema imefanikiwa kudhibiti maambukizi mapya kwa wajawazito kwani kati ya watoto 197 waliozaliwa kutoka kwa akina mama wenye maambukizi ni mtoto mmoja tu ndiye ameambukizwa.

Kufuatia changamoto hiyo kuripotiwa baadhi ya wawakilishi wa wananchi na viongozi wa kada mbalimbali akiwemo Tumaini Mtewa na Nikson Nganyange ambao ni madiwani wa halmashauri ya mji wa Njombe wamewahimiza wananchi wanaotumia dawa kufuata taratibu za matumizi ya dawa hizo na kuwa wafuatiliaji wa wenzao wanaojaribu kutoroka kwenye dawa. 

Baadhi ya wananchi akiwemo Roida Mbilinyi wamekiri kupokea elimu waliyopewa na wataalamu wa afya na kwamba wanakwenda kuhimiza ndugu jamaa na marafiki waliopo kwenye matumizi ya dawa kuzingatia maelekezo.

Mkoa wa Njombe ungali kinara kwa maambukizi ya Ukimwi kitaifa kwa kuwa na asilimia 11.4 ukifuatiwa na mkoa wa Iringa wenye asilimia 9.1 na Mbeya yenye asilimia 9.0

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI