Header Ads Widget

ENG. KUNDO: NITAUJENGA NA KUUNG'ARISHA MJI WA BARIADI.

 

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Bariadi Mjini kupitia CCM, Mhandisi Kundo Mathew (katikati) akiwa kwenye Mkutano wa kampeni mtaa wa Kidinda Mjini Bariadi.


Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Bariadi Mjini kupitia CCM, Mhandisi Kundo Mathew, amesema kuwa endapo atachaguliwa Oktoba 29, kuwa Mbunge atahakikisha anaendelea kuleta na kusimamia fedha za miradi ya Maendeleo ili kuweza kuung'arisha na kuujenga Mji wa Bariadi ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Simiyu.


Aidha, Mhandisi Kundo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi kumchagua Mgombea Urais Dk. Samia Suluhu Hassan na madiwani wanaotokana na Chama hicho ili waendelee kufanya kazi ya kuwaletea Maendeleo.


Akizungumza kwenye Mkutano wa kampeni uliofanyika Mtaa wa Kidinda, kata ya Bariadi, Mhandisi Kundo amesema serikali ya CCM itaendelea kuboresha miundombinu ya Afya, Elimu, Maji, Barabara na Umeme, ikiwa ni pamoja na kuweka taa katika mnada wa Kidinda, kupanua daraja la mnadani, na kurekebisha barabara ya Gulioni–Malinoni.


Pia ameahidi kufungua barabara za mtaa wa Buzunza na Nyangaka, kuongeza umeme katika kaya za pembezoni, na kupanua tanki la maji ili kuongeza upatikanaji wa maji ya Ziwa Victoria.


"Shukrani zetu tukazionyeshe kwenye sanduku la kura...Mpinzani wetu ni changamoto za wananchi wetu, tunataka kujboresha Mji wa Bariadi na kuisuka ifanane tutaongeza taa 60, tunaendelea kufungua Barabara za mitaa ili kuboresha Mji wa Bariadi" amesema.





Akiwa Mtaa wa Kilulu kata ya Bunamhala, Mhandisi Kundo ameahidi kuboresha daraja la Mto Mwalala, kujenga zahanati mpya katika mtaa huo, na kuboresha chanzo cha maji ili kuhakikisha upatikanaji wa maji safi. 


Mhandisi Kundo ametumia mikutano hiyo kuwanadi na kuwaombea kura Wagombea Udiwani wa CCM kutoka kata za Bunamhala (Nkamba Zabron) na kata ya Bariadi (Michael Gimbuya).


Mwisho. 









Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI