NA GIFT MONGI MATUKIO DAIMA APP MOSHI
Kufuatia ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa mbili katika kijiji cha Sembeti kata ya Marangu Mashariki wilaya ya Moshi kulikopelekea vifo vya watu watano umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi(UVCCM)wilayani hapa wametuma salamu za rambi rambi kufuatia tukio hilo.
Jengo hilo la ghorofa lililokuwa lilikijengwa liliporomoka usiku wa Desemba 18 na kusababisha vifo vinne papo hapo ambapo walifunikwa na kifusi huku mwingine akikutwa na umauti akiwa hospitali akiendelea na matibabu.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenail Shirima amesema umoja huo umepokea Kwa masikitiko makubwa kufuatia tukio hilo kwani walipoteza maisha wakiwa kwenye harakati za kujitafutia kipato katika njia halali.
"Kwa masikitiko makubwa tumepokea taarifa za tukio hilo ambalo limepoteza vijana watano ambao bado taifa liliwahitaji hivyo nitoe pole nyingi kwa familia za wapendwa wetu"amesema
Amesema wengi waliokumbwa na tukio hilo ni vijana na kuwa ni pigo kubwa kwa kundi hilo ikizingatiwa kuwa kuna wategemezi wao wameachwa nyuma ambao wamebaki katika kipindi kigumu.
Shirima amewataka vijana wilayani Moshi kuendelea kuungana kwa pamoja katika kipindi hiki kigumu ambacho wamewapoteza wapendwa wao huku serikali ikiendelea na taratibu nyingine kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Kamanda wa Polisi Kilimanjaro Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema jengo hilo lilikuwa linajengwa na mafundi walikuwepo jumla ya watu thelathini .
"Jengo hilo lilikuwa linajengwa na wafanyakazi walikuwa 30, wafanyakazi 5 wamefariki na 9 kujeruhiwa na wanapatiwa mtibabu,marehemu mmoja bado hajafahamika hivyo wananchi wanapaswa kwenda kutambua mwili huo,bado jengo hilo linafukuliwa zaidi"amesema
Kwa mujibu wa kamanda Maigwa ni kuwa watu wote waliopoteza maisha ni wanaume ambao ndio walikuwa mafundi katika jengo hilo la ghorofa mbili
Mkuu wa wilaya ya Moshi Abbasy Kayanda ambaye pia ni kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro amesema kwa sasa kamati inaenda kuundwa ilu kuweza kubaini chanzo cha ajali hiyo.
0 Comments