Header Ads Widget

LATRA YAITAKA TRC KUPANGA NAULI WATAKAZOMUDU WANANCHI TRENI YA SGR

Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam

Mamlaka ya udhibiti wa  usafiri Ardhini (LATRA) imetoa mapendekezo ya nauli za treni ya mwendokasi (SGR) iwe bei ambayo mwananchi wa kawaida ataweza kuimudu Ili kuweza kupata abiria wengi zaidi.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa LATRA Habibu Suluhu alipokua katika Mkutano wakupokea maoni ya wadau kuhusu nauli zilizopendekezwa na TRC amesema kuwa, watumiaji wa huduma hiyo ni watu wa chini sana hivyo lazima trc walizingatie hilo.


"TRC walituletea mapendekezo kuhusu nauli z treni ya SGR tukayapokea sasa leo tumekutanisha wadau wa usafiri ardhini Ili wawaeleze mapendekezo hayo lakini wazingatie kuhusu maisha ya wananchi waeke bei ambayo kila  mwananchi ataweza kuimudu"amesema Habibu.


Aidha, amesema kuwa mapendekezo yaliyotolewa na TRC kuhusu nauli za treni ya SGR ni kwa daraja la kawaida kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ni shill 24,794 kwa mtu mzima na mtoto kuanzia miaka4 - 12 ni shill 12,397 ambapo daraja la kati kwa mtu mzima shill 29,752 na mtoto ni shill 14,876.


"Mapendekezo ya Nauli ya tren ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa daraja la kawaida kwa mtu mzima ni shill 59,494 na mtoto kuanzia miaka 4 hadi 12 ni shill 29,747 na daraja la kati ni shill 71,392 kwa mtu mzima na mtoto ni shill 35,696"amesema Habibu.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ngw'ilabuzu Ludigija wakati akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala katika Mkutano huo amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imelenga kuboresha miundombinu ikiwemo barabara Ili kuweza kumrahisishia mwananchi katika harakati za kimaendeleo.


Aidha, ameiomba LATRA kutoridhia mapendekezo hayo mpaka wananchi watakapo yakubali kwani wao ndio watumizi wakubwa, huku akiwataka wananchi kutoa maoni yao ya mapendekezo ya nauli kwa lengo la kupata muafaka wa nauli bora ambayo mwananchi ataweza kuimudu.

Naye, Kaimu Katibu Mtendaji LATRA CCC, Leo Ngowi amesema kuwa ikiwa nauli itakua  juu hakutakua na abiria atakae hitaji usafiri huo, hivyo TRC itapoteza apato na Biashara zinazoweza kushamiri kama vile migahawa, mabenki, usafiri pamoja ajira.


Aidha, amesema kuwa ni vyema TRC wakapanga bei za kawaida ambazo wananchi wanaweza kuzimudu na wakaomba ruzuku Serikali na kurudi kutoa mapendekezo na kujadiliwa upya kwani zaidi ya abiria 53 asilimia 100 waliohojiwa walisema gharama ni kubwa hawawezi kuzimudu.


"Ushauri na mapendekezo ya baraza baada ya kufanya uchambuzi wa kina kuhusu nauli pendekezwa, tunaiomba LATRA irudishe nauli zilizoombwa na TRC kwa lengo la kufanya maboresho, endapo watapata idhini ya ruzuku ya Serikali wawasilishe maombi upya kwa ajili ya kujadiliwa tena na wadau"amesema Ngowi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI