Header Ads Widget

RAS MTWARA AHIMIZA JAMII KULINDA WATOTO WENYE ULEMAVU

 



Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Abdallah Malela amesema kuwa kila mmoja anawajibu wa  kuhakikisha kuwa anawalinda watoto wenye ulemavu kwakuhakikisha kuwa wanapata haki zao stahiki ikiwemo kupata elimu.


Kauli hiyo ameitoa katika semina ya siku moja iliyoandaliwa Shirika lisilo la kiserikali la Child Support Tanzania kwakushirikiana na Mtandao wa Asasi zisizo za Kiserikali Mkoani Mtwara MTWANGONET amesema kuwa watoto wenye ulemavu wanapaswa kuuangaliwa na kusaidiwa.


“Na sisi ni wadau wakubwa ambao tunawajibu wa kuhakikisha kuwa haki zao zinapatikana naimani kubwa huu mkutano utakuwa na tija kubwa kwa mkoa wetu natarajia wadau muhimu wapo hapa na tutaangalia haki za binadamu na mifumo watoto wenye ulemavu katika elimu jumuishi”


“Watoto wenye ulemavu wanahaki ya kutunzwa kulindwa dhidi ya ukatili unyanyasaji na kuwawezesha kuishi vizuri kama watoto wengine tunawajibu wa kutoa elimu kwa jamii ili kuwasaidia watoto hao” alisema Malela



Nae mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali la Child Support Tanzania Edward Majura alisema kuwa wadau wamekaa na kujadili namna gani bora ya kuweka ulinzi kwa watoto wenye ulemavu ikiwemo na kusimamia haki zao ikiwemo kuhamasisha waende shule.


Alisema kuwa tunahamasisha ili watoto wenye ulemavu waweze kupelekekwa shuleni ili kuhakikisha mtoto mwenye ulamavu akilindwa


“Hawa watoto wamekuwa wakifanyiwa vitendo mbalimbali vya unyanyasaji  ndio  maana tumeweka mikakati ili kuhakikisha kuwa jamii inapata elimu stahiki juu ya kusadia watoto wenye”



Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Asasi zisizo za Kiserikali Mkoani Mtwara MTWANGONET Fidea Luanda alisema kuwa katika semina hiyo wanaangali nini wanaweza kufanya ili kuhakiksiha kuwa watoto wenye ulemavu wanakuwa salama na kutoka katika mazingira magumu yanayowakabili.


“Tumekuwa tukitekeleza miradi mbalimbali ya kielimu ambapo tumeona vijijini zipo changamoto nyingi zaidi ya mjini ambapo tunaangalia uwajibikaji  pesa nyingi zinapelekwa katika shule ili kuangalia matumizi sahihi ya fedha hizo je  malengo yanatimia zinafika shule na kufanya shughuli iliyokusudiwa na jamii inashiriki vipi maendeleao ya shule” na maboresho yakoje tumefanya pia na shule zetu zenye mahitaji maalum Mtwara teck, Shangani na Rahaleo”




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI