Header Ads Widget

DC MTWARA AWATAKA WATENDAJI KUTOA ELIMU YA LISHE KWENYE MIKUTANO YA KIJIJI

 





Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kutoa elimu ya lishe kwa jamii kwakutumia njia mbalimbali ikiwemo kwenye mikutano na mashuleni.  


Ameyasema hayo wakati akishuhudia uwekaji wa saini katika mikataba ya lishe baina ya Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara  na Watendaji Kata  pamoja na watendaji Kata na watendjai Na vijiji  ambapo amesema kuwa ili kuwa na jamii yenye afya lazima elimu itolewe ili iweze kuwafikia na wajue aina gani ya chakula wanapaswa kula na chakula gani ni mlo kamili ili waweze kuzingatia.



“Wafundisheni vizuri waelewe hata ikiwezekana wekezi mpaka bustani za mbogamboga mashuleni pia himizeni wananchi walime kwaajil ya kuboresha afya zao ili tuweze kuondokana na udumavu lazima tuwahimize kuzingatia elimu tunayowapa pamoja na ushauri tunaotoa” alisema Kyobya


Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Erica Yegela  alisema kuwa mikata hiyo  itaenda kupunguza changamoto za utapia mlo na udumavu  wa mwili na akili pamoja na kuwaondolewa wajawazito tatizo la kujifungua watoto wenye vichwa vikubwa  na migongo wazi.


“Katika mikataba hii mnaenda kusimamia  nna kutoa elimu ya masuala ya lishe kwa wananchi na kuwahimiza kulima mazao mbalimbali ikiwemo mbogamboga na matunda” 



“Lengo ni kuboresha hali ya lishe na kupunguza utapia mlo katika jamii hasa mimba inapotungwa na motto kufikisha miaka miwili kwa siku tunahesabu siku 1000 lengo ni kuondoa udumavu wa mwili, akili, wanawake kujifungua watoot wenye vichwa vikubwa na migongo wazi”


“Tumeweka mikakati ili kuhakiksiha kuwa jamii inakuwa na uelewa juu ya masuala ya lishe ili kupugnuvuza udumavu wa akili na mwili” alisema Yegella




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI