Header Ads Widget

RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA KIKWETE AONGOZA KIKAO HIKI KIZITO

 


Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya  Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Masuala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education (GPE) ameongoza Vikao vya Bodi ya Taasisi hiyo vinavyofanyika Jijini Paris,  nchini Ufaransa kuanzia tarehe 5 hadi 7 Disemba, 2022.  


Vikao hivyo ni vya kwanza vya ana kwa ana tangu dunia ilivyokumbwa na ugonjwa wa COVID-19 mwishoni mwa mwaka 2019.  


Katika vikao hivyo, Taasisi ya GPE inapitia na kuazimia masuala mbalimbali yatakayolenga kuboresha mifumo ya elimu katika nchi zinazoendelea ikiwemo kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata elimu, wakiwemo watoto wa kike, na matumizi ya teknolojia katika utoaji wa elimu.




Akiwa nchini Ufaransa kwenye Mkutano wa Bodi Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia maswala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education - GPE) ambayo yeye ni 

Mwenyekiti, Rais Mstaafu Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazunguzo mafupi na Mheshimiwa Amadou Ba, Waziri Mkuu wa Senegal. Katika mazungumzo hayo, masuala ya elimu yaligusiwa, kati ya masuala mengine.


Akiwa nchini Ufaransa pembeni ya Mkutano wa Bodi Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia maswala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education - GPE) ambayo yeye ni 

Mwenyekiti, Rais Mstaafu Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazunguzo mafupi na Bi.  Audrey Azoulay, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO).   Katika mazungumzo ya viongozi hao, imekubaliwa kuwa UNESCO na GPE zitaendalea kushirikiana katika kupeleka ajenda ya elimu mbele.











Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI