Header Ads Widget

RAIS DKT.SAMIA AMETOA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 16 ZA MABORESHO SEKTA YA AFYA MKOA WA SONGWE.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi Cha Shilingi Bilioni 11 ambazo zimefanikisha kukamilika kwa Ujenzi wa Hospitali mpya ya rufaa Mkoa wa Songwe na Ujenzi wa Hospitali za Wilaya.


Hatua hii imesaidia Wananchi wa Mkoa wa Songwe kuepukana na kadhia ya kusafiri takribani km 75 mpaka Mkoa wa Mbeya kufuata huduma jambo lililokuwa likiwasababishia Mzigo wa Gharama na Vifo.


Kwa Sasa Rais Dkt Samia amefanikisha na kuwezesha Hospitali ya rufaa Songwe kutoa huduma za kibingwa huku ikisheheni majengo ya kisasa na Vifaa tiba.


Kwa upande wa hospitali za Wilaya Rais Dkt.Samia ametoa Shilingi Bilioni 2.3 kwaajili ya Ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Ileje, Wilaya ya Songwe Bilioni 2.3, Wilaya ya Momba Milioni 900 na Wilaya ya Mbozi jambo lililosaidia kusogeza huduma karibu na Wananchi.


Katibu tawala wa Mkoa wa Songwe Happiness Seneda kwa niaba ya Wananchi wa Songwe anamshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mapinduzi na Maboresho makubwa aliyoyafanya kwenye sekta ya Afya Mkoani humo na anaahidi kuwa kila fedha inayotolewa Kwaajili ya miradi ya maendeleo itatumika kwa lengo lililokusudiwa na kusimamiwa ipasavyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS