Header Ads Widget

KILIMO CHA UMWAGILIAJI MKOMBOZI KWA WAKULIMA DODOMA

NA HAMIDA RAMADHAN DODOMA

KILIMO cha Umwagiliaji ni aina ya msingi ya kilimo kwani ina mfumo wa umwagiliaji na hutumia njia tofauti za asili na bandia kwaajili ya kumwagilia. 


Aina zote hapa zinahitaji maji endelevu Mojawapo ya mifumo inayojulikana ya umwagiliaji ni umwagiliaji wa matone ambapo ni lazima  mkulima kumwagilia kwa kila siku ili mmea uweze kupata maji na kuzaa mazao kwa wingi.


Kama tunavyojua Mkoa wa Dodoma ni moja ya Mikoa kame ambayo katika historia ya hali ya hewa inajulikana Mkoa huo upata mvua yake Mara moja kwa Mwaka .


Hali hiyo imekuwa ikisababisha Mkoa huo kuwa na uhaba wa Chakula kutokana na wakulima kulima kwa juhudi na mvua kukata mapema.

 

Kutokana na hayo wakulima jijini Dodoma wameamu kubadilika na kuanza kulima kilimo cha umwagiliaji huku wakijivunia kuona manufaa ya kilimo hicho.


Kama tunavyofahamu wakulima wengi mwaka huu hasa katika mkoa wa Dodoma wameonekana kuchoka baada ya kulima kwa wingi na Mvua kukata au kusimamia mapema na kuacha mazao yakiungua jua.


Ni ukweli kwamba Wakulima jijini Dodoma wamekiri kuwa kilimo Cha Umwagiliaji ndio mkombozi wa wakulima tofauti na Kulima kwa kusubiri mvua za msimu.


Devid  Mtimbi Mwaka ni Mmiliki wa Shamba la Mbogamboga na Matunda (MTIMBIs FARMS) lililopo Chinangali Wilayani Chamwino ambapo ametoa ushauri kwa wakulima kubadilika na kuanza kulima kilimo cha kisasa cha umwagiliaji kwa kutumia Mbegu bora na kuwatumia wataalamu wa kilimo ili kuona tija ya kilimo.


Akiongea na Matukio Daima Blog  Devid Mtimbi Mwaka amesema shamba hilo tangu kuanzishwa ni mwaka wa pili na ni shamba lenye hekali 40 na wamekuwa wakilima kisasa kilimo cha umwagiliaji bila kutegemea mvua na kutumia wataalamu kulima kidogo faida kubwa.


Mwaka amesema Mkoa wa Dodoma umekuwa ukijulikana Kama Mkoa kame na Ardhi isiyokuwa na maji lakini ni tofauti kilimo katika Mkoa wa Dodoma kinawezekana kwani kila zao linakubali .

"Kikubwa hapa ni wakulima wapewe elimu juu ya kilimo cha kisasa cha umwagiliaji Mimi nimejionea Dodoma ni Mkoa wenye Ardhi yenye rutuba na mkulima anaweza kulima ndizi zikastawi kama zinavyostawi Mkoa wa kagera mafanikio katika kilimo yapo," amesema Mkulima Mwaka.


Sambamba ya hilo Mwaka ameishukuru Serikali na Wizara ya Kilimo chini ya Waziri wake Hussein Bashe kwa kuwapa mwanga na kuwa pamoja na wakulima na kuwapa mbinu mpya mabwana shamba juu ya kuwafikia wakulima na Kutoa elimu kulima kilimo cha kisasa.


Aidha amewashauri wakulima kuweza kununua mbegu kutoka Shirika la kimataifa la RIJK ZWAAN ambapo amesema wamekuwa na Mbegu nzuri zilizozalishwa kitaalamu na Mbegu hizo zimekuwa zikitoa mavuno mengi.


Kwa Upande wake Abel Kiley Mtaalamu wa kilimo mshauri kutoka Kampuni ya RIJK ZWAAN amesema Kampuni hiyo imekuja kuwapunguzia wakulima muda wa kukaa shambani na kulima eneo dogo mavuno yakutosha.


Amesema Kulima sio kukosea njia kulima ni sawa na mfanyabiashara anayefungua flemu ya duka mjni hivyo wakulima wanatakiwa kufahamu vizuri kilimo na taratibu zake lazima kujua mche mmoja utanipa kilo ngapi ya zao nitakapovuna.


Naiman Mollel kutoka Kampuni ya RIJK ZWAAN Tanzania kampuni ya Mbegu ya mbogamboga za Chotara amesema, katika upande wa kilimo wakulima wa Dodoma wamekuwa na changamoto kubwa hasa katika suala zima la uchaguaji wa mbegu sahihi na yenye matokeo makubwa.


Akiongea katika shamaba lingine la mfano lililopo Mlowa Barabarani Naiman amebainisha kuwa,wakulima wamekuwa wakichagua mbegu zisizo sahihi na ambazo hazina mazao mengi hata katika shamba dogo na hiyo yote ni kutokana na kukosa elimu ya wapi mbegu bora inapatikana na zenye uwezo mkubwa katika eneo .


Aidha ametoa wito kwa maafisa ugani kuacha kukaa maofisini na badala yake watoke kwa wakulima na kuwapa elimu ya namna bora ya kulima kilimo chenye tija kwaajili ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla.


"Ukweli ni kwamba Wakulima wanachangamoto kubwa kwani hawajui uchaguzi sahihi wa mbegu bora, kutaharisha shamba na kuandaa kitalu, pia amesema maji ni kiungo muhimu katika shamba hivyo maafisa ugani wawaelimishe wananchi namna ya kupata maji ili hata ikitokea mvua zimekata kilimo kiendelee na mazao yasiathirike kwa kukosa maji," alisema .

Wakiongea kwa nyakati tofauti tofauti wakulima hao wameishukuru Kampuni hiyo ya uzalishaji Mbegu bora na za kisasa RIJK ZWAAN .


"Niukweli usiopingika wakulima wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi hivyo kupatikana kwa mbegu bora na kuwatumia wataalamu wa kilimo tija itaonekana,"amesema.


Jackson Kawera  Mtunzaji wa shamba  la mfano huko Mlowa barabarani ameishukuru kampuni ya RIJK ZWAAN kwa kuzalisha mbegu nyenye ubora na tija kwa wakulima wamekuwa wakivuna mavuno mengi na vipato vyao vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku.


"Hapa changamoto kubwa katika Kijiji chetu ni ukosefu wa maji licha ya kuchimba visima lakini bado tatizo hilo limekuwa kikwazo kwetu," amesema Kawera.


Naye Shida Kisidi Mkazi wa Mlowa barabarani ameeleza kwamba kupitia shamba hilo wamepata ajira kuanzia uandaaji wa shamba hadi uvunaji wanapata fedha kwaajili ya kutunza familia na kusomesha watoto pia wamepata elimu ya kuweza kulima kilimo cha kisasa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI