Header Ads Widget

POLISI NJOMBE KUWEKA DORIA KILA KONA SIKU KUU YA MWAKA MPYA

 


Na Gabriel Kilamlya matukio DaimaAPP NJOMBE

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amesema jeshi la polisi limepanga doria katika maeneo yote ya miji ili kuhakikisha wananchi wanasherekea siku kuu hizo  kwa salama na amani.


Aidha Kamanda ISSA ametoa onyo kwa Madereva wa vyombo vya moto kuzingatia alama za barabarani Wakati wote hususani katika kipindi hiki Cha mwisho wa mwaka.


Pia wito umetolewa kwa watoto kulindwa na kuvushwa kwenye vivuko barabarani huku taa za barabarani zikitakiwa kuzingatiwa.


Vitendo vya kupiga na kulipua baruti, makopo na break fire za pikipiki zinazosababisha taharuki Wakati wa kuvuka mwaka ni navyo vimepigwa marufuku.


Katika taarifa hiyo Kamanda ISSA aliwaonya Walevi  kujiepusha na tabia hiyo Wakati wa kusherekea siku kuu hizo na kwamba ni bora kupumzika kunywa pombe katika kipindi hiki.


Sanjari na hayo jeshi la polisi limesema Makanisani pia kutakuwa na ulinzi wa kutosha hivyo ibada zitafanyika bila shaka yoyote.


Gari za IT zimetakiwa ziache tabia ya kubeba abiria kwani kufanya hivyo Ni kinyume Cha sheria  na Dereva atakayebainika atafikishwa mahakamani

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI