Teddy Kilanga _ Arusha
Naibu waziri wa Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi na utawala bora,Deogratius Ndejembi amewataka waajiri wote nchini kuajiri wataalamu wa ununuzi na Ugavi wenye sifa ili kuepusha mzigo wa lawama kwa baadhi yao pindi miradi inapokwama.
Kongamano hilo la 13 la mwaka la wataalam wa ununuzi na ugavi lililofanyikia jijini Arusha lenye lengo la kuwakutanisha na kuwaleta pamoja wataalam wa ununuzi na ugavi pamoja na wadau wengine wa ndani na nchi jirani ili kuweza kujifunza na kujadili changamoto ya masuala ya ugavi na ununuzi
Akizungumza katika kongamano hilo,Ndejembi alisema ili kuepusha malalamiko hayo ni vyema waajiri wote wakahakikisha wanaweka watu wenye sifa kusimamia idara za ununuzi na ugavi.
"Na panapotokea Mwajiriwa kakosa sifa wasisite kuwapeleka shule ili kuweza kujiendeleza wakiwaombea categorizationi na sisi tutajitahidi kuzifanyia kazi ikiwa lengo ni kupata watu wenye sifa katika sekta hii,"alisema Naibu Waziri huyo.
Aidha alisema ni vyema Waajiri wakazingatia mahitaji ya waraka namba 3 wa mwaka 2015 wa muundo wa utumishi wa kada zilizochini ya wizara ya fedha na mipango ambapo kada ya ununuzi na ugavi ni mojawapo ya kada zilizopo ndani ya waraka huo.
Aidha alisisitiza kuhakikisha watumishi waliopo katika kad hizo wanazo sifa za kitaaluma na waache utaratibu wa kutengeneza makundi ya ndani.
"Unakuta wakati mwingine Mtu yupo katika nafasi ya utendaji wa kata anapewa mafunzo ambayo sio sahihi alafu anapangiwa sekta ya ugavi na ununuzi katika kituo cha afya na mambo yakiharibika ndipo lawama zinapotokea,"alisema Ndejembi.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya wataalam wa ununuzi na ugavi (PSPTB)Godfrey Mbanyi alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 bodi ya ununuzi na ugavi imeendelea kusajili wataalam wake wapatao 1995 katika ngazi mbalimbali na kufikia jumla ya wataalam 15309 waliosajiriwa.
Pia alisema katika kusimamia ukidhi wa sheria bodi itaendelea kuchukua hatua madhubuti ya kudimamia weledi na maadili ya ununuzi na ugavi waliosajiliwa pamoja na kuchukua hatua za kisheria kwa wataalamu wasiosajiliwa.
"Bodi ipo katika hatua za awali za kuchukua hatua za kinidhamu ambapo bodi imekusudia kuwaita wataalamu 63 ili waweze kuchukua maelezo ili hatua mbalimbalo ziweze kuchukuliwa pamoja na kuchukua hatua za kalipio kwa wataalamu 78 ambao wamebainika kufanya kazi chini ya viwango,"alisema.
Naye mwenyekiti wa bodi hiyo Jacob Kibona alisema kuwa bodi imepewa jukumu la kisheria la kusimamia Wataalamu wa ununuzi na ugavi hii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba nchi yetu inakuwa na wataalamu wa kutosha wenye sofa stahiki na kufuatilia utendaji wao.
Alisema mara nyingi inapotokea changamoto kwenye miradi bila kujali muhisika alihusika katika kusimamia kutekeleza hatua hiyo maafisa ugavi ma ununuzi ndio pekee wanaoshitumiwa ambapo kufanikiwa kwa miradi kunategemea weledi wa ununuzi na ugavi ambo bodi hiyo inawasimamia na kuwalea kitaaluma hivyo hatua za kinidhamu ziweze kuchukuliwa kwa watu wote wa kada mbalimbali wanaohisika katika mradi huo.
0 Comments