Header Ads Widget

MNEC ATOA SALAMU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA KWA WATOTO YATIMA

 Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Ramadhani Mlao MNEC amewataka Watoto yatima kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan afya njema na umri mrefu katika kuwaongoza na kuwatumikia watanzania katika vipindi vyake vya uongozi.


Amesema hayo wakati akitoa salamu za heri ya Krismasi na Mwaka mpya katika vituo viwili vya watoto yatima vya AMANI ORPHANAGE CENTER na SYCAMORE CHILDREN'S HOME vilivyopo wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani alisema Rais ana majukumu makubwa katika taifa hivyo anahitaji kuombewa sana.


"Sisi Watanzania ndio wenye jukumu la kumuombea Rais wetu mpendwa ili aongoze nchi yetu vizuri na kuendelea kutuletea maendeleo" alisema Ramadhani.

Aidha aliwaambia Watoto hao kwamba Rais Dr. Samia yupo pamoja nao kwenye kila Hali.


Pia Ramadhani amewachangia Shilingi 300,000 kwa ajili ya kununua mifuko 20 ya Saruji katika kituo cha Amani Orphanage Center kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa mabweni  na kuahidi kutatua changamoto ambazo zimebakia.


Ramadhani akiwa katika kanisa la Parokia teule ya Makurunge na kuonana na Sister Yustina Edward Maganga ambaye ni Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha Sycamore children Home na kuweza kuwasilisha salamu zake za sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya.


Mwisho ametumia fursa hiyo kuwatakia watanzania wote heri ya Krismasi na Mwaka mpya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI