Header Ads Widget

MBUNGE APIGA JEKI UJENZI WA KITUO CHA POLISI

Mbunge wa jimbo la Buhigwe Felix Kavejuru akizungumza katika moja ya mikutano yake na wananchi.

Mkuu wa polisi kata ya Janda wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma I Ispekta  Chrisant Geroge (kulia) akitoa maelezo kwa Mbunge wa jimbo la Buhigwe Felix Kavejuru (wa tatu kulia) kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kituo cha kisasa cha polisi kwenye kata hiyo wakati mbunge na viongozi wa CCM walipotembea kuona maendeleo ya mradi huo ambapo Mbunge ameahidi kutoa shilingi milioni tano za bati zinazohitajika kukamilisha mradi huo. 

(Picha na Fadhili Abdallah)


xxxxxxxxxxxxxxxxxx


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

MBUNGE wa jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma Felix Kavejuru ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni tano kuchangia ujenzi wa kituo cha kisasa cha polisi katika kata ya Janda wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.

Kavejuru alitoa ahadi hiyo alipotembelea kituo hicho kuona maendeleo ya ujenzi wake na kuridhika na hatua iliyofikia ambapo alisema kuwa gharama za kuezeka jengo lote la kituo hicho atatoa yeye.

Mbunge huyo alisema kuwa kituo hicho cha polisi ambacho kitakuwa na vyumba vya utawala, mahojiano na rumande madhubuti ityasaidia katika kuimarisha masuala ya ulinzi na usalama wa eneo hilo ili kuwezesha wananchi kufanya kazi bila hofu.

Awali kabla kuahidi kumlizia jengo hilo mbunge huyo ameshatoa kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya mchanga uliokuwa unatumika kujengea jengo hilo ambapo unatoka Kigoma Mjini.

Kwa sasa polisi wanatumia jengo la zamani lililochakaa ambalo majengo yake yanakaribia kuanguka yakiwa hayana mabahusu inayoweza kuhifadhi wahalifu sugu wala sehemu imara ya kuhifadhia silaha (Amari)/

Akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo kwa Mbunge wa jimbo la Buhigwe, Felix Kavejuru polisi jamii kata wa kata ya Janda wilaya ya Buhigwe, Ispekta Chrisant George alisema kuwa kwa sasa ujenzi wa jengo hilo umefikia uswa wa renta.

George alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho cha kisasa ni muhimu kwa ajili ya utendaji wa shughuli za ulinzi wa jeshi la polisi katika kata hiyo yenye wakazi 20,000 kikihudumia vijiji vitatu na vitongoji 12.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI