Header Ads Widget

MLINZI WA CHUO CHA RUCU IRINGA AKAMATWA KWA TUHUMA ZA WIZI WA GARI ,MWINGINE AFUNGWA MIAKA 30 KWA KUBAKA MTOTO

 


Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limewakamata watu 5 kwa makosa mbalimbali ikiwemo mwanamke mmoja (61) kukutwa na jino moja la Tembo na meno mawili ya Kiboko na mlinzi wa chuo kikuu cha Ruaha ( RUCU) Iringa  kwa kosa la wizi wa gari katika eneo lake la kazi.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa Habari na kusema kuwa katika tukio la kwanza mlinzi wa chuo kikuu cha RUCU David Richard (23) ,  amekamatwa kwa kosa la wizi wa gari aina ya Toyota Raum yenye no za usajili T702 DFV mali ya Abraham Gasper (34) mfanyabiashara na mkazi wa mkwawa.


Katika tukio lingine jeshi lapolisi kwa kushirikiana na askari wa uhifadhi wamefanikiwa kumkamata Benadetha Kipago (61) mkulima na mkazi wa Izazi akiwa na jino moja la tembo na meno mawili ya kiboko.



Aidha, Kamanda Bukumbi amesema  kutokana na taarifa za siri jeshi hilo limefanikiwa kumkamata Boni Kipalile mkulima na mkazi wa Igagidungu  anayetuhumiwa kujihusisha na matukio mbalimbali ya kihalifu akiwa na silaha moja aina ya shortgun yenye namba 14949 na risasi tatu moja ikiwa chemba.


Pia jeshi hilo limewakamata watuhumiwa wawili wanaojihusisha na matukio ya kihalifu ikiwemo wizi wa pikipiki ambapo katika maeneo tofauti waliwakata  watuhumiwa hao wakiwa na pikipiki tisa (9), ambao Alfred Mkanula (25) fundi pikipiki mkazi wa mseke alikamatwa akiwa na pikipiki sita (6)  n azote aina ya SANLG na mwenzake Emanuel Mnyeke (28) mkazi wa Zizi La Ng’ombe alikamatwa na pikipiki tatu (3) mbili aina ya BOXER na moja Homda  pamoja na spear mbalimbali za pikipiki


Hata hivyo kamanda Bukumbi ameelezea mafanikio ambayo jeshi la polisi mkoa wa Iringa wameyapata ni kutoka mahakamani ni mtuhumiowa Sebastiani Mahuwili (42) mkulima na mkazi wa Nzivi aliyekuwa anatuhumiwa na kesi ya kubaka amehukumiwa 6/12/2022 kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kutokana na kupatikana na kosa la kumbaka mtoto wa miaka sita.

Gari lililoibwa na mlimzi wa chuo Cha RUCU
Bastola ya kienyeji iliyokamatwa


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI