Header Ads Widget

MBUNGE BENAYA KAPINGA NA STELLA MANYANYA WAMPONGEZA RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN PAMOJA NA TANROADS - RUVUMA.

     Na Amon Mtega, Mbinga.

MBUNGE wa Jimbo la Mbinga Vijijini Benaya Kapinga pamoja na Mbunge wa Jimbo la Nyasa mhandisi Stella Manyanya wamewapongeza wahandisi wa Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) Mkoani Ruvuma kwa kusimamia kikamilifu ujenzi wa moja ya barabara za kimkakati kwa kiwango cha lami kutoka Kitai mpaka Lituhi.


 Akizungumza Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini Benaya Kapinga  amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo ilikuwa ni ndoto ya muda mrefu lakini sasa inatimia kupitia Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutenga fedha za ujenzi huo ambayo itawapunguzia adha Wananchi pamoja na kuinua vipato vyao.


Mbunge Kapinga ambaye wameongozana na Mbunge wa Jimbo la Nyasa mhandisi Stella Manyanya kwenda kuangalia ujenzi wa barabara hiyo inayotakiwa ikamilike ndani ya miezi 18 amesema wasimamizi wa mradi huo kutoka Tanroads Ruvuma wanafanyakazi yao ipasavyo ndiyo maana mkandarasi anaijenga kwa kasi.

 Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nyasa Stella Manyanya amesema kuwa barabara hiyo itakapokamilika itakuwa ni ukombozi kwenye jimbo hilo na kuwa itakuwa imefungua utalii kwa kasi zaidi pamoja na wakazi wa Wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe wataitumia kikamilifu .


Manyanya ameeleza kuwa Jimbo la Nyasa linavivutio vingi lakini baadhi yao wamekuwa wakishindwa kwenda kufanya utalii kwa sababu ya miundombinu ya barabara ilikuwa siyo rafiki kwa sasa miundombinu inaimalika ambapo ilianza barabara Mbinga -Mbambabay kwa kiwango cha lami sasa ni Kitai -Lituhi.


Naye msimamizi wa mradi huo kutoka Tanroads mhandisi Andrew Sanga amefafanua kuwa mradi huo kwa sasa mkandarasi kutoka kampuni ya China mkataba wake ni wa Kilometa 35 kutoka Amanimakolo hadi Luanda ambapo itagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 60 ikiwemo na ujenzi wa madaraja ambayo kwa sasa madaraja hayo yapo manne.

 Mhandisi Sanga amesema kuwa Serikali imetoa fedha hizo ili kuhakikisha mradi huo unakamilika na kuwa kazi yao nikusimamia kikamilifu kwa kuzingatia viwango vinavyostahili ambavyo vipo kwenye mkataba huku akisema taratibu za ujenzi wa barabara kutoka Luanda hadi Lituhi zinaendelea na Mwisho wa siku ujenzi huo utakamilika maeneo yote yaliokusudiwa.

 Pia mkandarasi aliyepewa kazi hiyo kutoka kampuni ya China Railway Seventh Group (CRSG) Ge Guanghuq amesema kuwa kilometa 35 hizo zitakamilika kwa wakati na kuwa kazi inaendelea kufanyika haijarishi kuwa ni msimu wa mvua.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI