Header Ads Widget

MADEREVA WANAOENDESHA VYOMBO VYA MOTO WAKIWA WAMELEWA WAPEWA ONYO


 Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi ,ARUSHA

Madereva wanaotumia vyombo vya moto wakiwa wamelewa katika Mkoa wa Arusha wamepewa angalizo endapo watabainika kuendesha magari hayo wakiwa wamelewa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha mratibu wa Polisi SP SOLOMON MWANGAMILO wakati akizumgumza na Madereva wa mabasi mapema leo Desemba 30, 2022 katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na Nchi jirani.

Mwangamilo amesema kuwa dereva atakayebainika ana viashiria vya pombe atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ambapo amewataka madereva wa magari hayo kutotumia vyombo hivyo wakiwa wamelewa.

Ameongeza kuwa kikosi hicho hakimkatazi mtu yeyote kutumia pombe ambapo amewataka madereva kufuata sheria na taratibu za usalama barabarani ili kuepuka mkono wa dola.

 

SP Mwangamilo amesema kuwa dereva atakayekamatwa kwa makosa hayo atafungiwa leseni yake na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa kuhatarisha Maisha ya watu na uharibifu wa miundo mbinu.

Sambamba na hilo amesema kuwa chanzo cha ajali nyingi ni ushabiki wa mwendo kasi ambapo amewataka madereva hao kuwapuuza wanaowashawishi kwenda mwendo kasi ili kuepusha ajali za mara kwa mara.

Kwa upande upande wake Bw. George Emmanuel ambae ni dereva amelishukuru Jeshi la Polisi hususani kikosi cha usalama barabarani kwa kutoa elimu na kuwakumbusha mambo muhimu ya kuzingatia Barabarani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS