Filamu ya Kitanzania inayoitwa Still Okay To Date? imefanikiwa kushinda Tuzo za Kalasha zinazoandaliwa na Bodi ya Filamu ya Kenya ambazo zimefanyika Nairobi.
Filamu hiyo imeshinda katika kipengele cha Best International Award kilichoshindanisha Filamu kutoka nje ya Kenya ikiwemo Filamu kutoka Uganda na nyingine tatu kutoka Tanzania.
Ma-Producer wa Filamu hii ni Kefa Igilo @kefa_ig akishirikiana na Jerryson Onasaa @code_Jerry na ndio ambao wamepokea Tuzo hizo.
Imeigizwa na Wasanii kibao akiwemo Elizabeth Chijumba (NIKITA) @nikita_chijumba, Tunu Mbegu na Dkt. Issa Mbura ambaye ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam idara ya sanaa bunifu. Waigizaji wengine chipukizi ni pamoja na Collins Frank na Catherine Michael ambao ni wahamasishaji maarufu wa mtandao wa TikTok
0 Comments