Header Ads Widget

WAVAMIZI WA MAENEO YA ARDHI BAGAMOYO WATAHADHARISHWA


 

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdallah amewataka wananchi wenye uhitaji wa kununua maeneo ya ardhi katika wilaya hiyo kujiridhisha mapema kwenye mamlaka husika za serikali kuepuka kujiingiza kwenye migogoro inayochochewa na baadhi ya watu hasa madalali wanaotumia nyaraka za kufoji kujitwalia maeneo wakishirikiana pia na baadhi ya watuishi wasio waadilifu.


Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kituo cha huduma za pomoja (One stop Centre) kuwakutanisha viongozi wa taasisi, idara na Mamlaka zote za serikali kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kusikiliza malalamiko na kero za wananchi.


Alisema malalamiko mengi ya wananchi ni ardhi watu kudhulumiwa maeneo yao, wengine kuuziwa maeneo ya serikali lakini sababu kubwa ni wengi wao kujinunulia maeneo kinyemela bila kujiridhisha kwenye mamlaka husika za serikali.


"Watu wamezoea kuvamia maeneo wakishavamia wanasubiri huruma ya serikali, lakini vyombo vya kisheria vinatoa maamuzi baadhi ya watu kutakiwa kuondoka kwenye maeneo ya ardhi lakini baadhi ya watu wanakaidi na kuendeleza maeneo hayo hayo ". DC-Zainab.



"Sisi tutakua wakali kwenye kusimamia sheria kinyume na hivyo haya mambo Bagamoyo hatutayamaliza kuna watu wanavamia maeneo, kuna wanaouza maeneo kiholela (Madalali) tena wengine wanafoji mihtasari na saini za viongozi lengo lao waweze kujitwalia maeneo ili wauze wapo ambao wapo ndani ya chama na wengine ni watumishi wa serikali kwenye hili nataka niwaambia tutasimamia haki”. Alisema Zainab Abdallah-Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo.


Alisema suala hilo lilishaanza kufanyiwa kazi ikiwemo na vyombo vya usalama ambapo wapo baadhi ya watu wanaofahamika watafikishwa kwenye vyombo mbalimbali ikiwemo mahakama kwa kuwa wanakabiliwa na tuhuma za kijinai (Kughushi nyaraka) na wengine ni watumishi hasa wa idara ya ardhi ambao wengine wamehamishwa ambao nao watalazimika kurejea kwa ajili ya kuwajibishwa.



Katika ufunguzi huo baadhi ya wananchi waliopata nafasi ya kutoa malalamiko yao moja kwa moja kwa mkuu wa wilaya, wengi wao madai yao ni sekta hiyo ya ardhi, wakisema kwa muda mrefu kuna mchezo wa baadhi ya watu kuvamia maeneo yanayomilikiwa na watu wengine, maeneo ya wazi na mengine yaliyopangwa kwa ajili ya huduma za kijamii (Kuzikia).


“Mfano mzuri Mhe.Mkuu wa wilaya mimi nilikua kiongozi wa eneo moja hapa Bagamoyo, tulikua na eneo tulitenga kwa ajili ya makazi ya milele (Makaburi) lakini lilivamiwa na tuliendesha kesi tukashinda hadi mahakama kuu, ninavyo kwambia sasa hivi kumejengwa Ghorofa”-Alisema mmoja wa wananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS