Header Ads Widget

TAMISEMI QUEENS MABINGWA LIGI YA MUUNGANO YA MCHEZO WA NETIBOLI MWAKA 2022

 


Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul  Novemba 03, 2022 Uwanja wa Jamhuri Morogoro amekabidhi Kombe kwa Timu ya TAMISEMI QUEENS ambao wameibuka  Mabingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa ya  Muungano mchezo wa Netiboli mwaka 2022,  baada ya kuifunga timu ya Kikosi Cha Valentia Zanzibar ( KVZ ) kwa jumla ya magoli 56 kwa 40.

Mhe.Gekul, pia amegawa vyeti na zawadi kwa wanamichezo bora, timu  zilizoshiriki pamoja na waamuzi wa  ligi hiyo.

Aidha,  ligi hiyo imepata timu ambazo zitashiriki Mashindano ya Afrika Mashariki mapema mwaka 2023 ambazo  kwa Tanzania Bara ni TAMISEMI QUEENS, JKT Mbweni, Nyika Queens, Magereza Tanzania (Morogoro)

Nyingine ni  kutoka Tanzania visiwani ambazo ni  KVZ, Zimatoto, Mafunzo na JKU, huku wanaume wakiwakiliswa na Bandari Veterans na Smart Boys

Mashindano hayo yalianza Oktoba 25, 2022 ambapo timu nyingine zilizoshoriki ni Mafunzo, JKT, Magereza, Nyika, Zimamoto, Kampala University, huku wanaume  wakishiriki kupitia timu ya  JKU Zanzibar, Samart Boys  pamoja na Bandari Veteran za Tanzania Bara.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS