Header Ads Widget

WADAU WA ELIMU WATAKIWA KUJITOKEZA KONGAMANO LA TLSB

 

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya huduma za Maktaba Tanzania TLSB Dkt Mboni A. Ruzegea akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani Leo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya huduma za Maktaba Tanzania TLSB Dkt Mboni A. Ruzegea akikabidhiwa kitabu na  Afisa habari na uhusiano wa TLSB

                            xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda (MB) anatarijiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la pili la kitaifa la huduma za Maktaba, Tamasha la vitabu na Usomaji litakalofanyika katika ukumbi wa mikutano Tanga Beach Resort and spa jijini Tanga.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya  huduma za Maktaba Tanzania (TLSB) Dkt Mboni A. Ruzegea amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kutoa fursa kwa wadau wote wa huduma za Maktaba nchini Tanzania kuweza kushiriki katika kongamano hilo, ambalo itakalofanyika Nov 23 hadi 24 mwaka huu.


"Pamoja na mambo mengine kongamano hili pia linatoa fursa kwa wadau kuweza kuchangia na kuamua kwa pamoja namna bora ya kuendesha huduma za Maktaba nchini Tanzania kwa maslahi mapana ya Taifa hili"amesema Dkt Mboni.


Aidha, amesema mada kuu itakayotolewa katika kongamano hilo"Mchango wa huduma za Maktaba, utunzaji nyaraka na Mafunzo ya ukutubi katika uboreshaji wa elimu Tanzania" ambapo kauli mbiu ni huduma za Maktaba kwa urithi wa kiakili na kiutamaduni katika maboresho ya elimu.


Sambamba na hayo bodi ya huduma za Maktaba Tanzania imewataka Waandishi wa vitabu,majarida kuhakikisha wanatii sheria na kanuni ikiwemo kupeleka nakala ya kazi zao Ili kusaidia kuweka kumbukumbu kwa kizazi kinachokuja.


Hata hivyo, amesema Serikali imetenga fedha kwa ajili kufanya ukarabati wa Maktaba Ili ziendane na hadhi ya maeneo ambayo yapo huku akitoa wito kwa wananchi na wadau wa elimu kujitokeza kwa wingi katika kongamano hilo.


Hata hivyo, amesema kongamano la kwanza la huduma za Maktaba na Tamasha la vitabu na Usomaji lilizonduliwa rasmi mwezi Novemba mwaka 2021 na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Juma Omari (MB) .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI