Header Ads Widget

ROMBO KUFIKIWA NA MATANGAZO YA DIRA YA DUNIA (DW)

Mwakilishi wa Dw nchini Tanzania Baltazari Kitundu.
 

Katika kuhakikisha kwamba jamii yote nchini Tanzania inafikiwa na matangazo ya Moja kwa moja ya dira ya Dunia( Dw )  ujerumani wamezindua program ya kurusha matangazo hayo ya Moja kwa moja kupitia Redio Banana fm iliyopo Moshi mkoani kilimanjaro.


Aidha Redio hiyo itasaidia  wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro na wilaya jirani ya Rombo na Same ambao wamekuwa wakisikiliza redio kutoka nchi jirani ya Kenya ambapo kwa sasa watafurahia matangazo hayo yatakayorushwa na kituo hicho moja kwa moja .


Baltazari Kitundu mwakilishi wa Dw nchini Tanzania amesema kuwa uzinduzi huo umekuja kutokana na kutokea mambo mbalimbali yakiwemo ya kisiasa ,covidi19, pamoja na mabadiliko ya Sheria ambayo yamebadilisha sera za Dw namna ya kupata mashirikiano kwenye redio Zilizopo kwenye nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania.


"Kwa hiyo baada ya hiyo kupata mshiriki mmoja Kama huyu ilikuwa ni sababu ya Msingi ya kusema sasa tumepita mapito mengi na angalau Sasa tumepata wa Kwanza wa kuendelea naye kwa hiyo tunasherekea kwa pamoja jambo Hilo"Alisema Baltazari.


Mkurugenzi wa Banana fm amesema kuwa kabla ya kuanzishwa kwa banana fm wananchi wa Rombo walikuwa hawapati matangazo ya Redio  Tanzania,kwani Redio nyingi zinazosikika kule ni redio za Kenya .


"Kwa hiyo nikaona nifanye kitu ili na sisi basi tusiwe Kama kisiwa tuwe sehemu ya baadhi ya watanzania na hiyo ndio sababu kubwa ya kurusha matangazo"Alisema.


Hata hivyo amewataka wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro hususani wa wilaya ya Rombo kuhakikisha kuwa wanaitumia vizuri redio hiyo kwani itaweza kuwasaidia katika shughuli zao ikiwa ni pamoja na kuwakuza kiuchumi na kijamii.


Kwa Sasa redio Banana fm inaskika katika mkoa wa Kilimanjaro,Tanga ,Manyara pamoja na Arusha .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI