Header Ads Widget

VIJANA TUNAAMINIWA.....MWENYEKITI UVCCM

 


Na Gift Mongi,Moshi

Vijana walioaminiwa katika serikali ya awamu ya tano na sita kwa kupewa nafasi mbali mbali ndani ya serikali wameonekana kufanya vyema jambo lililoonesha kuwa bado vijana waliopikwa wanao uwezo wa kuongoza.


Katika serikali ya awamu ya tano na sasa ya sita baadhi ya vijana wamepewa nafasi mbali mbali zikiwemo ukuu wa wilaya,ukuu wa mikoa,katibu tawala wa wilaya, katibu tarafa pamoja na nafasi nyinginezo 


Kwa mantiki hiyo vijana waliopewa nafasi hizo kwa kiwango kikubwa wamefikia malengo ya kile kilichokusudiwa jambo linaloashiria bado kundi hili ambalo ni kubwa kwenye jamii bado lina uwezo mkubwa katika uongozi.


Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa uchaguzi wa viongozi wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)ngazi ya mkoa,mwenyekiti wa umoja huo wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenali Shirima amesema  vijana bado ni hazina kubwa kwa taifa hili na uchaguzi uliofanyika leo ni pamoja na kuwapata viongozi sahihi watakaoongoza umoja huo.


Amesema vijana wana uwezo bado katika kulitumikia taifa hili na ndizo sababu hasa zimekuwa zikipelekea wao kuaminika katika kukabidhiwa majukumu makubwa kwani uwezo wao katika utendaji ni mkubwa


Akizungumzia kuhusu umoja huo amesema ni kama karakana ya kuwaandaa viongozi wa serikali na chama kwa kipindi kijacho hivyo ni vyema kuwa na viongozi ambao ni sahihi kwa afya ya umoja huo.


Katika uchaguzi huo mwenyekiti wa UVCCM  mkoa wa Kilimanjaro aliyemaliza muda wake Ivan Moshi ameweza kutetea tena kiti chake hicho kwa kipindi kingine cha miaka mitano kuanzia 2022-2027


Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa amemtangaza  mwenyekiti huyo ambaye amepata kura 492 kati ya kura 546 ambazo zilipigwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi.


Aidha mwenyekiti huyo Ivan Moshi amewashukuru wajumbe wa mkutano huo kwa kumuamini tena kwa kipindi kingine na kuwa vijana wanatakiwa kuzikimbilia fursa na sii kusubiri ziwafuate.


Aidha amewataka wenyeviti wa umoja huo katika ngazi za kata wasikubali kugombanishwa na watendaji na kuwa itawawia vigumu katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku katika kuleta maendeleo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI