Header Ads Widget

ST. JACOBUS YAJIPANGA KUINUA KILIMO

 


ESTHER MACHANGU_MOSHI.


Kukosekana na elimu ya Kilimo katika mitaala ya elimu nchini, kumechangia vijana wengi wanaohitimu  ngazi mbalimbali za elimu kusubiri kuajiriwa na si kujiari, hali inayopelekea kuwa na vinaja wengi mtaani wanaosubir ajira.


Wafadhili kutoka nchini Italia kwa kushirikiana na Kanisa Katoliki wameanzisha shule ya St.Jacobus technical and Agricultural science secondary school, Ili kutoa elimu yenye mafunzo ya kilimo ambayo yawasaidia wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo mbinu za kujiajiri na kuona umuhimu wa kuendeleza kilimo.


Naye mwakilishi wa Same foundation (Tasisi isiyo ya kiserikali kutoka nchi Italia)Dr. Antonio Bonetti amesema wao wejikita katika kuboresha Elimu ya kilimo kwa kushirikiana na Same Foundation wamelata matrekta pamoja na kufungua garage ya dhana hizo ambapo wanafunzi hao wanajifunza kuyatumia na pia kuyatengeneza.



Mthibiti ubora elimu Wilayani Same Calist Youze, amesema kwa sasa serikali imepunguza vigezo vya kuanzisha shule ambapo hapo awali wamiliki Binafsi walitakiwa kuwa na kiasi kisichopungua milioni 65,  heka 5 pamoja na mlolongo wa barua za kuomba kibali Cha kuanzisha shule.


Kwa upande wake Askofu Jimbo katoliki la Same Rogate Kimario amesema licha ya wao kutoa huduma Lakini wamekuwa wakikubwa na kadhia ya baadhi ya Tasisii za serikali kuwalazimisha kuwa na leseni za biashara.



Baadhi ya wanafunzi wa kidato Cha kwanza katika shule hiyo akiwemo Emanuel kanuti,Sister Maria Epifania wamesema elimu wanayoipata katika shule hiyo itawasaidia katika Kujikwamua kiuchumi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI