Wito huo umetolewa jana na mkurugenzi wa Kampuni ya( CF) Chesco Ng’umbi ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika mahafali ya saba katika chuo cha ufundi stadi R.D.O Mdabulo, Mufindi na kuelezea kuwa vijana wengi wanapohitimu masomo yao wanajikuta kuwa tegemezi kutokana na kutegemea kupata ajira jambo ambalo kwa sasa limekuwa ni gumu.
Chesco
amesema mafunzo ambayo wanafunzi wanayapata katika vyuo vya R.D.O hapa nchini
yanawezesha vijana kupata ajira kwa wakati au kujiari wenyewe kutokana na uzoefu
ambao hautegemei vyeti pakee.
Naye
mkurugenzi wa Rural Development Organization (RDO) Fidelis Filipatali amesema
chuo hicho kinajivunia mafanikio mbali mbali kwa jamii inayowazunguka tangu
kuanzishwa kwake miaka 20 iliyopita, kwani kimetoa misaada mbali mbali Pamoja kuwalipia
ada ya masomo wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu.
Aidha
Fidelis amekumbusha wahitimu hao Kwenda kufanya kazi kwa vitendo kama ambavyo
wamefundishwa chuoni hapo ili kuweza kupata ajira kwa wakati au kujiajiri
wenyewe.
Nao baadhi
ya wanafunzi waliohitimu mafunzo hayo wamekishukuru chuo cha ufundi stadi (RDO)
kwa msaada wa mafunzo waliyowapatia kwani wamefanikiwa kujifunza kwa vitendo
mafunzo mbali mbali ambayo yatawawezesha kukabiliana na changamoto ya ajira
inayoikabili dunia kwa sasa.
0 Comments