NA Zulufa Alfan Matukio Daima App Simiyu
Balozi wa Pamba Nchini Aggrey Mwanry ameutaja mkoa wa simiyu ndio unaongoza kwa ulimaji zao la Pamba Kati ya mikoa 17 na wilaya 56 inayolima zao Hilo Nchini
Amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakulima Busega mkoani Simiyu huku akiwataka baadhi ya wakulima kuacha tabia ya kutelekeza mashamba yao badala yake waweze kuandaa mashamba mapema hasa katika msimu huu wa kilimo.
Kwa upande wake mkuu Wa wilaya ya Busega Gabriel Zakaria anaomba wakulima wa zao la Pamba waweze kufikiwa na huduma kwa wakati Kama vile mbegu mbolea na dawa huku akitumia fursa Hiyo kuwaonya baadhi ya watendaji wa vijiji wasio waaminifu
0 Comments