Header Ads Widget

SHIRIKA LA UNFPA LA AHIDI KUFANYA USHIRIKINO NA SERIKALI YA TANZANIA

 




Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


KATIKA kuhakikisha wananchi wanatambua Matumizi sahihi ya Matokeo ya Sense ya watu na makazi iliyofanyika Agosti 23 mwaka huu Shirika La Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya Watu Duniani (UNFPA)limeahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutoa elimu 


Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dodoma mara baada ya kufanya mazungumzo na mwakilishi mkazi wa UNFPA Wilfred Ochuan ambaye anamaliza muda wake hapa nchini, Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Anne Makinda alisema matokeo ya sense yanatakiwa yalete tija kwa wananchi katika kufikishiwa shughuli za maendeleo na huduma za kijamii.


Alisema shirika lililosaidia  kufanikisha sensa ya Watu naakazi ni UNFPA kwasababu kimataifa wao ndio wanao simamia mambo ya idadi ya watu.


Amesema walikuwa wanasaidia kwenye mambo ya ufundi,vifaa na kuwashirikisha na mataifa mengine ikiwemo kupata vishikwambi 600 kutoka South korea, 200 kutoka UN WOMEN na China.


“Huyu Wilfred Ochuan ameteuliwa kwenda Ghana kuwa mwakilishi wa idadi ya watu hivyo alikuja kutuaga na kuaga wafanyakazi wa hapa”amesema Makinda.


 “Yeye ameahidi kwamba wataendelea kutusaidia ili watu waweze  kujua matumizi ya takwimu sasa hatuna mila sana ya kutumia takwimu lakini kwa sasa tunataka hilo liweze kuonekana kabisa”amesema.


 Pia amesema watatumia takwimu hizo kufanya mipango yao,ufatiliaji wa maendeleo mbalimbali ili ziweze kutumika kwenye bajeti ya serikali na waliahidi Euro laki 2.


“Tujaribu kutafuta mbinu zote watanzania tuanze kutumia hizi sensa ,kwani sensa zinagharama sana kwahiyo huwezi kufanya kitu kwa gharama halafu badae unakiacha tu”alisema.


Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt Albina Chuwa alisema Tanzania inawatu wakarimu kama ilivyo kwa wananchi wa nchi ya Ghana ambao nao pia sikuzote wameonekana wakarimu hivyo tunaimani utakwenda kutusaidia  kupeleka picha ya nchi ya Tanzania ilivyo .


“Bila shaka tunaimani  utachukua yale yote mazuri yaliyopo Tanzania kwani hata Rais wetu wa awamu ya sita samia Suluhu Hassan amekuwa akiishangaza dunia  kwa mambo makubwa anayoendelea kuyafanya”amesema.


Chuwa amesema katika suala zima la takwimu nchi ya Tanzania imekuwa bingwa na imeonekana ni nchi inayoendelea  kukuwa kiuchumi kwa takwimu za Afrika  .


“Mafanikio hayo yote yamekuja kutokana na kuwa na mawasiliano na  uwazi kwani ndio kitu kikubwa kwetuna pia tunajivunia kuwa na mtu kama mama Anna Makinda ambaye ndio aliyekuwa kamisaa wa sensa Tanzania bara”amesema.


Akizungumza Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa UNFPA anayemaliza muda wake Wilfred Ochang   aliishukuru serikali kwa kuweza kushiriki katika zoezi zima la sensa kwani ameweza kujifunza mambo mengi mazuri na makubwa juu ya masuala yote ya sensa.


 “Nawahakikishia kuwa naenda kupeleka mazuri yote yaliyomo na niliyoyapata katika nchi ya Tanzania, na hongereni kwa kuweza kufanikisha zoezi zima la sensa ya watu na kazi,”amesema.


 “ Kwa nchi ya Ghana tunakwenda kufanya sensa ya kidigitali mwezi mei 2023 japokuwa tumechelewa lakini tunaendelea kujifunza na hakika nitakwenda kupata uhakiki baada ya kukamilika kwa zoezi zima la sensa  ya kidigitali hivyo naomba ushirikiano kutoka kwenu, ”amesema




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI