NA TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima App.
JESHI la Polisi Mkoani Kagera limefanikiwa kuwaua watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi katika mipaka ya wilaya ya Ngara na Biharamulo mkoani Kagera.
Hayo yamesemwa na kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa kagera, ACP William Mwampagale wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa jeshi hilo lilifanya operashani maalumu baada ya kupata taarifa kuwa kuna kundi lililokuwa linapanga kufanya uhalifu.
" Jeshi la polisi mkoani kagera lilifanya operasheni na msako mnamo Novemba 15 mwaka huu kufuatia taarifa za kiintelijensia kuwa kuna kikundi cha majambazi kimepanga kufanya uhalifu kwa kutumia silaha na mnamo mwezi Novemba 15, 2022 tuliweza kuweka mitego katika maeneo hayo ambapo watatu wenye jinsia ya kiume wanaosadikiwa kuwa majambazi kujeruhiwa kwa risasi wakati wa majibizano ya risasi kati yao na
Jeshi la polisi hivyo wakati wanakimbizwa hospitali walipoteza maisha na miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Ngara Nyamiaga"
Amesema majambazi hao walikuwa watano jinsia ya kiume waliokuwa wanakadiliwa kuwa na umri wa miaka 25-35 na katika uchunguzi wa awali uliofanya na jeshi hilo umebaini kuwa kikundi cha watu hao kimekuwa kikifanya matukio ya unyang'anyi wa kutumia silaha tangu mwezi Septemba na Oktoba mwaka huu katika maeneo ya kijiji cha Bugarama,Muganza na Murusagamba.
Hata hivyo Mwampagale ameongeza kwa katika operashani hiyo wamefanikiwa kupata silaha moja aina ya AK47 isiyokuwa na namba pamoja na magazine moja ikiwa na risasi 12 na hivyo kutumia nafasi hiyo kuwaonya wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Sambamba na hilo jeshi la polisi mkoa wa Kagera amewataka wananchi wa mkoani humo kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa sahihi za uhalifu pamoja na wahalifu ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao kabla ya madhara kutokea.
0 Comments