Header Ads Widget

SASA TUNAJIPANGA KWA 'VIJANA GREEN MARATHON'.....

 


Na Gift Mongi,Moshi


Vijana wa chama cha mapinduzi(UVCCM)wamesema mara baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa ngazi ya mkoa kwa jumuiya hiyo sasa maandalizi ni kwa ajili ya mbio za 'Vijana Green Marathon'zinazotarajiwa kufanyika novemba 26.2022 jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa umoja huo wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenali Shirima amesema maandalizi yote yapo tayari na kuwa vijana wameonesha mwitikio mkubwa katika kushiriki mbio hizo zenye lengo la kuutangazia umma mambo mema yanayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita.


Amesema vijana ambao ndio jeshi kubwa wamehamasika katika kushiriki mbio hizo kwa kuwa wengi wao wamekuwa ni wanufaika wa mambo mbali mbali ambayo yanatekelezwa na serikali kwa sasa.


Kwa mujibu wa Shirima ni kuwa mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi ndani ya jumuiya hiyo sasa wanao muda muafaka katika kushiriki mbio hizo ambapo pia viongozi wa kitaifa wa jumuiya hiyo watakuwa wameshaoatikana.



Akizungumzia kuhusu umoja huo amesema ni kama karakana ya kuwaandaa viongozi wa serikali na chama kwa kipindi kijacho hivyo ni vyema kuwa na viongozi ambao ni sahihi kwa afya ya umoja huo.


Katika uchaguzi uliomalizika hivi karibuni  mwenyekiti wa UVCCM  mkoa wa Kilimanjaro aliyemaliza muda wake Ivan Moshi aliweza kutetea tena kiti chake hicho kwa kipindi kingine cha miaka mitano kuanzia 2022-2027


Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa alimtangaza  mwenyekiti huyo ambaye amepata kura 492 kati ya kura 546 ambazo zilipigwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi.


Aidha mwenyekiti huyo Ivan Moshi amewashukuru wajumbe wa mkutano huo kwa kumuamini tena kwa kipindi kingine na kuwa vijana wanatakiwa kuzikimbilia fursa na sii kusubiri ziwafuate.


Aidha amewataka wenyeviti wa umoja huo katika ngazi za kata wasikubali kugombanishwa na watendaji na kuwa itawawia vigumu katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku katika kuleta maendeleo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI