Na Shomari Binda-Musoma
UCHUNGUZI wa magonjwa ya moyo kwa mara ya kwanza yameanza kufanyika mkoani Mara katika "clinic"ya madaktari bingwa ya Royal iliyopo mjini Musoma.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufanyiwa vipimo na uchunguzi, baadhi ya wagonjwa wameshukuru kwa kupatikana huduma hiyo.
Wamesema katika kipindi cha nyuma wamekuwa wakitumia gharama kubwa kwenda mikoa ya mbali kupata huduma hiyo lakini kwa sasa imewafikia.
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Musa Mafuru,amesema amekuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo kwa muda mrefu na amekuwa akisafiri hadi hospital ya taifa Muhimbili kufanya uchunguzi.
Amesema kwa sasa anashukuru huduma hiyo kupatikana mkoani Mara kwa vipimo ambavyo amekuwa akisafiri kuvitafuta mbali.
" Clinic ya Royal kwa kweli imetuletea huduma nzuri ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo ambayo kwa upande wangu ni muhanga wa tatizo hili.
" Nimekuwa ukitumia gharama kubwa kwenda Muhimbili kupata huduma lakini kwa sasa ntakuwa nikizipata hapa kwenye clinic ya Royal",amesema Musa.
Mganga mfawidhi wa Royal Polyclinic, Hosea Bisanda,amesema mashine hizo za uchunguzi wa magonjwa ya moyo zimefunuliwa kwa gharama ya milioni 60 na zina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 80 kwa siku.
Amesema licha ya kuanzisha kitengo cha uchunguzi wa magonjwa ya moyo lakini pia wameanza kutoa huduma za Echo,ECG,Utra Sound na hivi karibuni wataanza kutoa huduma za kinywa na meno pamoja na macho.









0 Comments