Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Peter Joseph Serukamba amefanya ziara ya kikazi wilaya ya Ikungi katika kijiji cha Choda kata ya mkiwa jimbo la singida mashariki ambapo alipata nafasi ya kuzungumza na wajumbe wa halmashauri ya kijiji pamoja na kusalimiana na wananchi wa kijiji cha choda
RC Serukamba amelazimika kuzungumza na halmashauri ya kijiji cha Choda katika kuhakikisha anaumaliza mgogoro wa viongozi wa kijiji hicho mara baada ya baadhi ya wananchi na viongozi kumuomba aingilie kati utata wa mgogoro huo
Akizungumza na viongozi hao Rc Serukamba amesema kwa mujibu wa maelezo aliyoyapata kutoka kwa viongozi wa halmashauri ya kijiji, pamoja na viongozi wa ccm wa tawi na kata amebaini tuhuma zinazotolewa dhidi ya mwenyekiti wa kijiji hicho hazina mashiko ya kumuondoa katika nafasi yake
Awali Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro akitoa taarifa ya jinsi walivyoshughulikia mgogoro huo amesema walilazimika kufanya vikao vitatu vya kutatua changamoto hiyo ambapo katika kikao cha mwisho mwezi Oktoba Dc Muro aliwataka kufuata utaratibu endapo wanaona tuhuma za kumtoa mwenyekiti wa kijiji zina ukweli jambo ambalo baadhi ya viongozi hawakufanya hivyo
RC Serukamba mbali na kupongeza jitihada za awali za wilaya katika kutatua mgogoro huo amewataka wajumbe wa halmashauri ya kijiji na viongozi wa ccm tawi kufanya kazi na mwenyekiti huyo na kumpa ushirikiano ili atekeleze majukumu yake ipasavyo na kuwaonya baadhi ya wajumbe kuacha kuweka maslahi yao binafsi
0 Comments