Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Balozi.Dkt.Batilda Salha Burian ameshiriki katika Mjadala wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia ,mjadala uliofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora .
Mkoa wa Tabora umeshiriki kwa njia ya Zoom(Mtandao) katika Mjadala wa Kitaifa juu ya Nishati Safi ,salama na endelevu kwa ajili ya kupikia ,mjadala uliongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Akiwakaribisha Wajumbe wa Mkoa wa Tabora Mhe.Balozi Batilda Burian alitoa shukrani kwa Mhe.Rais Samia kwa kuanzisha mjadala huu wa kitaifa ambao unaenda kulinda afya za Wananchi pamoja na kulinusuru Taifa dhidi ya Ukataji holela wa Miti pamoja na uharibifu wa Mazingira .
"Tabora tunamshukuru na kumpongeza Mhe Rais kwa kuanzisha Mjadala huu wa Kitaifa kuhusu Nishati safi, salama na endelevu kwa ajili ya kupikia. Kwa hakika Mama ni Mama tu. Amezidi kukonga nyoyo za wananzego". RC Batilda
Aidha Mhe.Balozi Batilda alieleza kuwa Takwimu za Mkoa zinaonesha kati ya Wagonjwa 132 walioripotiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Kitete katika kitengo cha Magonjwa ya Ndani wagonjwa 66 sawa na asilimia 50 wameathirika kutokana na matumizi ya Kuni na Mkaa .
0 Comments