Header Ads Widget

POLISI DODOMA KUWEKA MIKAKATI YA KUTOKOMEZA VITENDO VYA KIKATILI

 

Na  Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma

JESHI la Polisi mkoa wa Dodoma limeweka mikakati mbalimbali ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto ikiwemo matukio ya ulawiti kwa watoto wa shule za msingi ambayo yameshika kasi siku za hivi karibuni.


Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Martin Otieno, alibainisha hayo jijini hapa  alipokuwa akitoa taarifa ya ushiriki wa jeshi hilo katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili zinazoanza Novemba 25 hadi Desemba 10 kila mwaka.


Amesema, duniani kote leo yameanza maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukali wa kijinsia hivyo wao kama jeshi la polisi wamepanga kushiriki kwa kufanya shughuli mbalimbali katika jamii.


“Leo (nchi zote duniani zimeanza maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia hivyo sisi kama jeshi la polisi tumejipanga kuendesha shughuli mbalimbali ambazo tutazifanya katika siku hizo zote”amesema


Kamanda Otieno, amesema jeshi hilo mkoa wa Dodoma pia wamepanga kutoa elimu kwa jamii kuelimisha kuhusu madhara ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.


“Tunapanga kuwa na utaratibu wa kutoa elimu ili kuhamasisha jamii kuachana na vitendo vya ukatili, tutakwenda katika maeneo ya nyumba za ibada, shule, sokoni, nyumba kwa nyumba na hata katika vyombo vya usafiri kutoa elimu kwa kushirikiana na dawati la jinsia mkoa”amesisitiza


Amesema moja kati ya matukio ya ukatili ambayo yanaripotiwa mara nyingi katika mkoa wa Dodoma ni ubakaji hivyo anatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia pamoja na matukio mengine ya kiharifu.


Aidha, amesema lengo la jeshi la polisi mkoa wa Dodoma kutumia siku hizo 16 kutoa elimu ni kiiwezesha jamii kutambua madhara ya vitendo vya ukatili na kuchukua hatua ya kukabiliana navyo.


“Lengo lingine ni kuhakikisha kuwa jamii inakuwa na uelewa ili kuweza kukemea ukatili katika jamii inayotuzunguka”amesema


Kadhalika, amesema katika siku hizo 16 watashiriki maadhimisho ya siku ya walemavu ambayo kimkoa yamepagwa kufanyika Desemba 3, mwaka huu wilayani Mpwapwa.


“Vilevile tumepanga kutembelea nyumba za kutunza watoto pamoja na wale wenye uhitaji na kutoa misaada mbalimbali, kutoa mafunzo kwa askari wetu kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia”amesema


Mmoja wa wakazi wa jiji la Dodoma Michael Mwafute, alisema ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini kila mtu anapaswa kuwa na hofu ya Mungu.


“Hivi sasa matukio ya ukatili wa kijinsia yamekithiri sana kila unaposikiliza vyombo vya habari unasikia mtu kamuua mke wake au kiongozi wa dini kamlawiti mtoto hii yote ni kukosa hofu ya Mungu”amesma Mwafute

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI