MKOA wa Pwani umepiga marufuku uvunaji wa mazao ya Misitu bila ya vibali ambapo watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini Mjini Kibaha.
Kunenge alisema kuwa changamoto kubwa ya ukosefu wa maji imetokana na uvunaji holela wa Misitu na uharibifu wa vyanzo vya maji.
Alisema kuwa Misitu ni chanzo kikuu cha kusababisha mvua kunyesha lakini baadhi ya watu wamevuna miti kwa kiasi kikubwa na kusababisha mvua kuacha kunyesha hivyo wale wote wanaofanya shughuli hizo waache mara moja.
Aidha alisema kuwa watachukua hatua kali ikiwa ni pamoja na kutaifisha vyombo vinavyotumika kusafirishia bidhaa zitokanazo na Misitu na wananchi kuangalia shughuli nyingine za kuwaongezea kipato.
0 Comments