Ng'ombe zaidi ya 375 wamekamatwa ndani ya Hifadhi ya Ruaha katika Bonde la Usangu /Ihefu majira ya saa mbili usiku Jana Tarehe 07/11/2022 ,Hii ni mbinu Mpya ya wafugaji kuingiza Mifugo usiku wakiamini askari wa uhifadhi watakuwa wamelala.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo cha Ikoga Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya Afisa Uhifadhi wa TANAPA Benedict Mwageni amesema Jeshi la Uhifadhi litafanya kila jitihada ya kuhakikisha shughuli za kibinadamu hazifanyiki katika bonde hilo
Mwageni amewataka wananchi waache kuingiza mifugo ndani ya hifadhi kwa kuwa nchi iko kwenye mgao wa umeme unaosababishwa na Mto Ruaha kukauka pamoja na wanyama kukosa maji jambo linalopekea vifo
Hata hivyo Ng'ombe hao waliokamatwa wanasubiri kutambuliwa na Wafugaji huku taratibu za kisheria zitafuatwa ikiwemo kufikishwa mahakamani.
0 Comments