Header Ads Widget

NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII MHE MWANAIDI APONGEZA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII RUNGEMBA

 


Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia,wanawake na makundi maalumu Mhe. Mwanaidi Ali Khamis  amepongeza maendeleo makubwa ya chuo Cha maendeleo ya Jamii Rungemba wilaya ya Mufindi mkoani Iringa na kuahidi kuendelea kutatua changamoto mbali mbali za chuo hicho .


Akizungumza Leo wakati wa Mahafali ya 34 ya chuo hicho alisema Kuwa atajitahidi kupitia wizara yake na wizara ya fedha kuendelea kutafuta fedha Kwa ajili ya maendeleo ya chuo hicho .


Alisema kuwa Raus Samia Suluhu Hassan aliunda wizara ya maendeleo ya Jamii kufanya kazi hivyo wito wake kuona maofisa maendeleo ya Jamii wanakwenda Vijijini kufanya kazi ya uelimishaji juu ya maendeleo ya Nchi pamoja na lishe Bora Kwa jamii.


Kuwa Kwa kufanya hivyo kutasaidia jamii kutambua haja ya kujiendeleza Katika fani ya maendeleo ya Jamii .


"Mnajua kwamba ukatili wa kijinsia umezidi Sana na Leo Novemba 25 ni siku ya uzinduzi wa siku 14 za kupinga ukatili wa kijinsia nchini wito wangu Kila mmoja kushiriki kupinga ukatili wa kijinsia "


Aidha akiwataka wazazi kutenga muda wa Kuelimisha watoto juu ya kutambua vitendo vya kikatili na kuepuka vishawishi vya wale wanaofanya vitendo vya ukatili.


Alisema kuwa lengo la Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuunda wizara hiyo ya maendeleo ya Jamii na kuona wizara inakuwa Mkombozi .

Pia aliwataka wahitimu pindi watakapopata kazi kufanya kazi Kwa weledi na kuepuka Rushwa pindi watakapokuwa kazi .




















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI