Klabu ya Mwanza Press Club (MPC) leo Novemba 16 imepokea ugeni toka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na kufanya mazungumzo mafupi ya namna ya kufanya kazi kwa pamoja kwenye eneo la kujengewa uwezo waandishi wa habari juu ya kuandika habari za uhaba wa chakula kwa mazao ya uvuvi/ Food Loss and waste Assessment
Maafisa hao ni Julie Heye na Omar Penarubia, ambao walishiriki kikao na baadhi ya viongozi wa MPC pamoja na wanachama.
Mambo mengine yakiyojadiliwa ni pamoja na waandishi wa habari kutumia jarida la FAO kuchapisha habari za chakula pamoja na umuhimu wa FAO kusaidia kundi la waandishi wa habari kwenye kutumia teknolojia kwenye kutekeleza majukumu yao.
0 Comments