Header Ads Widget

MBUNGE ANNE KILANGO AANZISHA MRADI WA VITI KILA KATA KUSAIDIA KIPATO KWENYE CHAMA CHA MAPINDUZI.

 


NA WILLIUM PAUL, SAME.


MBUNGE wa Jimbo la Same mashariki wilayani Same mkoani Kilimanjaro, Anne Kilango Malecela ameanzisha mradi wa ukodishaji viti kwa kila kata za Jimbo hilo kupitia chama cha Mapinduzi lengo likiwa ni kuondoa dhana ya chama kuwa tegemezi na kuombaomba.



Akizungumza katika hafla ya kukabidhi viti hivyo jana, Mbunge huyo amesema kuwa lengo la kuanzisha mradi huo ni kuhakikisha chama kinakuwa na mradi wa kujipatia kipato ili kufanya wepesi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 pamoja na uchaguzi Mkuu 2025.




Alisema kuwa, viongozi wa Chama ngazi ya kata wamekuwa wakipata wakati mgumu hasa kipindi cha uchaguzi kutokana na kukosa fedha za kampeni hali ambayo imekuwa ikipelekea kuomba kwa watu mbalimbali hivyo kuja kwa mradi huo utaondoa dhana hiyo.


"Jimbo langu linakata 14 ambapo kila kata nimeipa viti vya plastiki 100 ambapo wao viongozi watakuwa wakivikodisha kwa wananchi na pesa itakayopatikana kupitia mradi huu itatumika katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu 2025" alisema Anne Kilango.



Mbunge huyo aliwataka viongozi wa Chama ngazi za kata kushirikia na viongozi wa matawi katika kutulinda na kuuendeleza mradi huo na kutoa wito wa kutokuwa mwanzo wa mafarakano na migongano baina ya viongozi na wanachama.



Katika kuhakikisha fedha hizo zinaweka mahali salama, Mbunge huyo alijitolea elfu hamsini kwa kila kata kwa ajili ya kufungua akaunti ya benki kwa kila kata ambapo fedha za ukodishaji viti zitakapokiwa zikihifadhiwi.




Aidha aliahidi kwa kata ambayo itafaya vizuri katika mradi huo wa viti ataiongezea idadi ya viti lengo ni kuhakikisha anaweka hamasa kwa viongozi kulinda miradi hiyo.


Alisema kuwa, lipo tatizo kubwa la usomaji wa taarifa za mapato na matumizi ya vijiji kwa wananchi ambapo amewataka viongozi wa Chama kata kuhakikisha wanawasimamia Wenyeviti wa vijiji kuhitisha mikutano ya hadhara na kusoma mapato na matumizi.



"Swala la usomaji taarifa za mapato na matumizi kwa vijiji hili ni tatizo kubwa kila mahali na huku kwenye Jimbo langu nimeona nisipowahi mapema kuja kulipatia ufumbuzi litanisimbua 2024 na 2025 na sijui kwanini hawataki kusoma hii taarifa" alihoji Mbunge Anne Kilango.

Na kuongeza "tumekubaliana kwa pamoja na viongozi wa Chama kata na matawi wakawasimamie Wenyeviti wote kuhitisha mikutano ya hadhara na kusoma taarifa ya mapato na matumizi mpaka ifikapo Disemba 31 mwaka huu kila mmoja awe amefanya hivyo sasa yule ambaye atashindwa kufanya hivyo atatueleza vizuri nini sababu".

Mwisho...

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI