Header Ads Widget

MNEC RUVUMA HEMEDI CHALLE ATINGA OFISI ZA WAANDISHI RUVUMA NA KUTOA NENO

 .

MNEC Ruvuma  akivijaribu moja ya  vifaa  vya studio ya Redio ya waandishi wa habari mkoa wa Ruvuma inayoendelea matengenezo.
Makamu mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Ruvuma Amon Mtega akielekeza jambo kwa Mnec juu ya ufanyaji kazi kwenye ofisi hiyo.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

         Na Amon Anania, Ruvuma.

MJUMBE wa Halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi CCM Taifa kupitia mkoa wa Mkoa Ruvuma (NEC)Hemedi Ahmad Challe amewataka Waandishi wa habari Mkoani humo kuendelea kuwa na mshikamano wa kuihabarisha jamii kwa mambo mbalimbali ikiwemo kutangaza miradi inayotekelezwa na Serikali iliopo madarakani.


  Wito huo ameutoa alipotembelea ofisi ya waandishi wa habari Mkoani humo iliyopo mkabala na Soko kuu la Songea majengo ya Hanga kata ya Mjini Manispaa ya Songea.


  Mjumbe huyo ambaye amechanguliwa hivi karibuni na wanachama wa CCM  kwa zaidi ya kura 600 amesema kuwa vyombo vya habari vimekuwa msaada katika kuhabarisha jamii hivyo ni vema waandishi wakaendelea kushikamana.


 Aidha katika hatua nyingine mjumbe huyo ametumia nafasi hiyo  kuwashukuru wanaccm wote  (Wajumbe)wa mkoa huo waliompa ridhaa ya kuitumikia nafasi ya NEC Taifa na kuwa hatawaangusha katika uwakilishi huo na akiwaombea kwa Mungu waendelee kuwa na Afya njema na kukitumikia chama hicho kwa uaminifu ili kizidi kusongambele huku akisema uchaguzi umeisha kilichobaki ni kufanya kazi.


 Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Ruvuma  Amon Mtega wakati akimshukuru mjumbe huyo kwa kutembelea ofisini hapo amesema kuwa vyombo vya habari vya mkoani mara zote vimekuwa vikihabarisha jamii pamoja na kutangaza miradi inayotekelezwa na Serikali .


 Mtega amesema kuwa licha vyombo vya habari na waandishi wake mkoani humo kutangaza miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali lakini bado wamekuwa wakishiriki shughuli mbalimbali kwenye jamii.


 Hata hivyo Mtega kwa niaba ya waandishi wa habari mkoani humo amempongeza mjumbe huyo kwa kuchaguliwa na wanaccm  kuitumikia nafasi ya NEC Taifa.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI