Header Ads Widget

CHAMA CHA MSINGI LINDI CHASHINDA PIKIPIKI KATIKA DROO YA BONGE LA MPANGO MCHONGO WA KUSINI NA NMB.

 

NA HADIJA OMARY,LINDI

CHAMA  cha Msingi cha Mandwanga AMCOS kilichopo Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi  kimejishindia pikipiki moja kupitia Droo inayoendeshwa na Benki ya NMB inayoenda kwa jina la BONGE la mpango  mchongo wa kusini.


Droo hiyo ya wazi imefanyika  leo Novemba 24, 2022 katika ofisi za Benki ya NMB Manispaa ya Lindi Mkoani Lindi na kushuhudiwa na wateja wa benki hiyo.


Hata hiyo droo hiyo iliendeshwa pia na kuwapata washindi wa mtu mmoja mmoja waliojishindia kiasi cha shilingi laki moja moja ambao ni Renatha and Dastan, Ramadhani Joseph Kowelo na Amir Tindwa kutoka Wilaya ya Mbinga , Bashiru Mteka  na Bakari Mbinga kutoka Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi.


Akizungumzia kampeni hiyo Meneja huduma kwa wateja wa NMB Lindi, Eyya Ngollo alisema Kampeni hiyo inalenga kuhamasisha wakulima mmoja mmoja pamoja na vyama vya msingi kuendelea kupata huduma katika benki ya hiyo.


Alisema kwa upande wa vyama vya msingi  (AMCOS) kampeni hiyo inashindanisha pikipiki huku kwa mtu mmoja mmoja ikishindanisha pesa taslimu kiasi cha shilingi laki moja ambapo kampeni hiyo itafanyika mpaka mwishoni mwa mwezi Disemba 2022.


Kwa upande wake Meneja mauzo NMB kanda ya kusini Roman Degeleki alisema droo hizo zimekuja  mahususi kwa ajili ya wakulima wa korosho katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo NMB imepanga kutoa pikipiki tano kwa vyama vya Msingi vya Ushirika vitakavyoshiriki katika Droo hiyo katika msimu huu wa mauzo ya korosho 2022/2023.


Alisema Droo ya Pikipiki hizo zitachezeshwa katika droo tano mfululizo kwa kila wiki ili kuwapata washindi kutoka katika vyama vya msingi Amcos kutoka katika Mikoa hiyo ya Lindi na Mtwara ambapo hiyo ni droo ya pili kufanyika.


Hata hiyo Degeleki alieleza kuwa  ili Chama kiweze kuingia kushiriki katika droo hiyo kinatakiwa kiwe na akaunti ya NMB pamoja na kupitisha mauzo katika akaunti hiyo ambapo chama kitashindanishwa kutokana na miamala inayofanywa na chama husika.


Naye  kaimu mrajisi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Lindi secilia Sostenec aliwapongeza Benki ya NMB kwa kuanzisha kampeni hiyo kwani ni moja ya motisha kwa vyama vya msingi ambavyo vinahudumiwa na Benki hiyo pamoja na wakulima.


“vile vile pikipiki hizo zitakazotolewa kupitia mchezo huu wa kubahatisha zitaweza kusaidia katika uendeshaji wa vyama kufuatilia mambo mbali mbali kwenye chama , kufuatilia wakulima, malipo pamoja na makusanyo ya Korosho na hata ufuta” Secilia.


“lakini pia nitoe wito kwa NMB kuendelea kuvisaidia vyama vyetu kwa mambo mbali mbali kama vile vitendea kazi kama kompyuta na vitu vingine kwa  sababu vyama hivi ndio wadau wakubwa kwenye Benki yetu ya NMB”.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI