Header Ads Widget

MIMBA ZA UTOTONI MIKOA YA KANDA YA ZIWA ZIMEZIDI

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma

IMEELEZWA Hali ya Vitendo vya Ukatili na Mimba za Utotoni katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ipo kwa kiwango cha juu hivyo serikali na wadau wametakiwa wote kushirikiana Ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo.


Mkurugezi wa Shirika la Kivulini linalojishughulisha na Mapambano Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia na Mimba za Utotoni lenye Makao yake Makuu Jijini Mwanza  Yasini Ally amesema hayo jijini Dodoma Novemba 8 ,2022 wakati alipokuwa akifanya mahojiano na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari Juu ya utendaji kazi wa shirika lake.


Mkurugenzi huyo  amesema Utafiti uliofanywa na Shirika Ilo umebaini katika kipindi cha mwaka 2015/ 2016 vitendo vya ukatili wa kijinsia Ulikuwa kwa hali ya Juu ambapo mkoa wa shinyanga ni asilimia 78, mkoa wa Mwanza asilimia 60 , mkoa wa Kigoma asilimia 61 na wakati mkoa wa Mwanza pia una asilimia 25 kwa vitendo vya mimba vya utotoni.


"Hali hiyo pia inaweza kusababishwa pale jamiii ya kanda ziwa inapokuwa na hali nzuri ya kiuchumi kwa mfano wakati wa mavuno baadhi ya watu utelekeza familia na kwenda Kwenye mambo ya starehe na kusababisha tatizo la mapenzi na makuzi katika familia zao," Alisema Mkurugenzi huyo.


Mkurugezi huyo ameongeza kuwa shirika hilo limefanya kazi kubwa ya kujenga uwezo kwa klabu za wanafunzi Ili kudhibiti mimba za utotoni ambapo pia Alisema Serikali na wadau wengine hawanabudi kuwekeza nguvu katika vitendo vya ulawiti kwani vitendo hivyo vimekuwa vingi katika jamii.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI