Header Ads Widget

MADEREVA MSIKUBALI KUVUTWA NA SHETANI:RTO ARUSHA

 


Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha mrakibu wa Polisi SP SOLOMONI MWANGAMILO amewataka madereva wa vyombo vya moto kuwa makini katika matumizi ya vyombo hivyo Pamoja nakufuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali za mara kwa mara katika Mkoa wa Arusha.


Hayo yamesema leo November 08 2022 wakati wa kukabidhi pikipiki kwa viongozi wa dini kutoka Manyara,Kilimanjaro Pamoja na Arusha ambapo amesema kuwa viongozi wanaowajibu wa kutibu mioyo ya wanadamu kiroho ambapo amewaomba kutokubali kuvutwa na shetani wakati wa matumizi ya vyombo hivyo.


SP Solomon amesema wao kama Jeshi la Polisi wanawajibu kutoa Elimu kwa makundi yote ili kuwa na uelewa wa Pamoja ili kukomesha ajali katika mkoa wa Arusha.


Kwa upande wa Askofu mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk BARNABAS MTOKAMBALI amesema lengo la kutoa vyombo hivyo ni kuwafikia waamini wa dhehebu hilo nakutoa huduma ya kiroho na kazi za kanisa ikiwa ni Pamoja nakuongeza kasi ya maendeleo ya kanisa hilo


Wakati huo huo Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha SP SOLOMON MWANGAMILO amewata madereva wa vyombo vya moto maarufu mando wanaofanya safari zao nje ya jiji la Arusha na Kwenda maeneo ya vijijini kufanya marekebisho ya vyombo hivyo ili kupunguza ajali za mara kwa mara.


Ametoa kauli hiyo katika kata ya Meserani wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha alipokuwa anazungumza na madereva wa vyombo hivyo ambapo amewataka kufanya marekebisho na kufuata sheria za usalama barabarani ili kuondoa ajali za mara kwa mara katika eneo hilo zinazosabishwa na vyombo hivyo maarufu Mando.











Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI