Header Ads Widget

MENEJA WA TRA MTWARA AWATAKA WAFANYABIASHARA KULIPA KODI

 Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Mtwara Naomi Mwaipola amesema kuwa taasisi hiyo haipo kwa ajili ya kuonea mtu hivyo kuwataka wafanyabishara kulipa kodi ili kuchagiza maendeleo ya nchi.


Akizungumza katika hitimisho la wiki ya mlipakodi Mkoani mtwara alisema kuwa taasisi hiyo inalengo la kukusanya zaidi ya milioni 56  ambayo tunaamini tutaifikisha kwa ushirikiano na wafanyabishara.


“Walipakodi wengi hawajui sheria za kodi japokuwa wanajitahidi kuzitafuta wala hawajui jinsi ya kutunza kumbukumbu wengi hawezi kuweka kumbukumbu za kuwawezesha kulipa kodi sahihi”


“Katika hatua nyingine tumebaini kuwa ipo changamoto ya matumizi ya mashine ya EFD ambapo kuna baadhi ambao hawatumii kabisa mashine hizo hawapendi kutumia mashine hizo”

Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Idara ya Upelelezi wa Kodi Felisiana Nkane  alisema kuwa lengo  la kukusanya shilingi bilioni 56. “Ipo mikakati ya namna ya kukusanya mapato tunapokea pia michango ili tuweze kuboresha mapato katika nchi yetu tunayo mikakati ambayo itawezesha mkoa wa mtwara kufanya kazi ipaswavyo”


Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Kanal Patrick Sawala alisema kuwa endeleeni kuwa karibu na walipa kodi na kuwa karibu na wananchi ili wazidi kuelewa na kuchangia kodi yao.

“Natambua kuwa lipoongezeko kubwa la ukusanyaji wa mapato mafanikio haya yametokana na maadili yetu na elimu mnayotoa kwa walipa kodi kwa kuboresha miundombinu hivyo kupunguza ukwamishaji wa ulipaji wa kodi”


“Pamoja na mafanikio bado zipo changamoto ambazo baadhi ni wafanyabishara kutotoa risiti za EFD na  kutolipa malimbikizo ya kodi na usalama katika mipaka ya Msumbiji”

“Lengo letu kubwa ni kuongeza ukusanyaji wa kodi nawahimiza hakikisheni mnaelimisha na kuhamasisha ulipaji kodi uweze kulipwa kwa wakati” alisema Kanal Sawala

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI