Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Zaidi ya Wakazi 1000 wa kijiji cha Utweve kata ya Ukwama wilaya ya Makete mkoani Njombe wanatarajia kuepukana na changamoto kubwa ya kupanda milima na kushuka pindi wanapotafuta maji baada ya serikali kuanza kutekeleza mradi wa zaidi ya shilingi milioni 304.
Utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 75 ambapo meneja wa Ruwasa wilaya ya Makete MHANDISI INNOCENT LYAMUYA amesema pindi utakapokamilika utakwenda kuwa Suluhu ya tatizo la maji kwa wananchi kijijini humo.
Tibery Sanga,Toba Ilomo na Christopher Sanga Ni wakazi wa kijiji cha Utweve ambao wamekiri kuwapo kwa adha kubwa ya upatikanaji wa maji hivyo kujengwa kwa mradi huo kuna waondolea adha hiyo kubwa.
Mkurugenzi mkuu wa Ruwasa Nchini MHANDISI CLEMENT KIVEGALO amesema ni lazima mapinduzi ya miradi bora ya maji ianzie Makete ambako anatokea Katibu mkuu wa wizara ya maji kwani haiwezekana eneo wananchi wake wakaendelea kutaabika kwa miaka mingi.
Diwani wa kata ya Ukwama Emmanuel Sanga amesema kilio cha maji kwa wakazi wake kimekuwa ni kikubwa na hivi sasa furaha yao imeanza kuonekana baada ya mradi huo kufikia hatua nzuri.
0 Comments