Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dr Geofrey Mkamilo ameagiza kituo cha Utafiti Naliendele kufanya tafiti zingine mpya ili kupunguza changamoto ya magonjwa na wadudu zinazojitokeza katika kipindi cha mabadiliko ya tabia nchi.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa mkutano wa kufanya tathimini ya kazi zinazofanywa na kituo hicho ambapo alisema kuwa mabadiliko ya tabia nchi hayapaswi kuzungumzwa kawaida kwa kuwa yameongeza wadudu magonjwa kwenye zao la korosho.
“Unajua unyevunyevu hewani husababisha kusambaza ugonjwa wa ubwiliunga kwenye mikorosho hata ukiwa na mvua kidogo kuliko mategemeo ni mabadiliko ya tabia nchi mara nyingine joto unakuta kali sana”
“Kuwepo kwa changamoto nyingi za zao la korosho tunahitaji kuweka miundombinu bora ya utafiti wa korosho kwa kujenga maabara ya kisasa ili tuweze kuzitumia kwa kugundua aina za magonjwa na wadudu katika zao hilo unaweza kumuona mdudu ukadhani ni ubwiliunga kumbe sio yeye lakini kupitia utafiti kwenye maabara ya kisasa tunaweza kutambua aina za wadudu” alisema Dr Mkamilo
Nae Mkurugenzi wa TARI kituo cha Naliendele Dr Furtunus Kapinga alisema kuwa Mambo mengi yanazuka wale wadudu waliokuwa sio tatizo lakini leo hii ni tatizo ule ugonjwa ambao ulikuwa hauna athari unaanza kuwa na athari.
“Tumeambiwa kuwa kuna maeneo panya wanapanda juu ya mbaazi wanakula mbaazi zikiwa juu hii inaonyesha kuwa hawa panya walizoea kupata vitu ambavyo hawavipati wanakula hata vitu ambavyo hawajawahi kula” alisema Dr Kapinga
0 Comments